Rev Kishoka ,nakushukuru kwa kulitambua hilo. Ni mengi umeyaongea na ya msingi. Ukichunguza zaidi maneno yako hayapingani hata kidogo na yale ya watu makini kama F.A.Mbowe,Mzee Mtei na Mh.Dr Slaa. Nakumbuka kwa nyakati tofauti wamesisitiza kuwa hawana uhasama na kikwete,hawana uhasama na mtu isipokuwa wanachopigania ni ule ufisadi,uzandiki,upuuzu na kutowajibika. Haya kwa pamoja ni mapungufu makubwa ktk serikali ya Kikwete. Kwa ufasaha zaidi uyu mkwere ni fisadi kama mafisadi wenzake aliwataja dr.slaa pale mwembeyanga lakini haimaanishi kuwa si lolote,hapana. Jambo kuu ni kwamba pamoja na rais kuwa na tuhuma binafsi,yeye angesimama kwa kofia ya mkuu wa nchi kulinda taifa lake,haijalishi rais ameingia vp ikulu,taifa linamhitaji kwa asilimia mia,ila kama anakuwa mzembe hatuna budi kumkumbusha na kutoa maoni yetu kama watanzania katika kutawala raslimali zote za taifa. Kwa upande wa pili kama si kulindana na kulipa fadhila kuna watu hawakupaswa kuendelea kumsaidia rais ktk kuitawala nchi,ni hatari kwa mtu aliyeshindwa majukumu auditable na kupewa majukumu abstrative,ni hatari. Kama rais anaipenda nchi yake na abebe mzigo wake asikimbie lawama. Nami nampongeza kikwete ila kwa ujumla sitakaa nimkubali kama mtenda kazi,amekumbatia wahujumu uchumi,waliofoji vyeti,wanyonyaji na wadhaifu,kwa aya Jk ni msaliti kwa umma na sitakaa nimuone kama kiongozi mahiri katika historia ya Tanzania tangu awe mbunge,waziri mpaka kiranja mkuu wa inchi. Kwangu hafai kuitwa kiongozi. Ni msimami wangu milele!