Shukrani kwa Kikwete


Kama ni hivyo, kwa nini usiwe mmoja kati ya waliochaguliwa, kama Kikwete vile, ili utuwekee hiyo mizani itakayo balance.
 
kazi gani?

kuanguka majukwaani na kupata sababu za kwenda kuzurura hospitali za ulaya na marekani nazo ni kazi?

watu wengine mna mawazo ya k*h*n*t** kweli.

Shule za sekondari kila kata ya Tanzania, zahanati kila kata ya Tanzania, mabarabara mikoa yote kaunganisha na sasa anaanza za wilaya, vyuo vikuu 11 kwa miaka 5, Zanzibar migogoro kwisha, Vibopar wizi wako mahakamani kibao, exemptions za kanisa zote kwisha funga. Jee niendelee na swali lako kazi gani?

Hayo matusi mimi sikujibu kwani wenye matusi hujulikana ni kina nani hapa kwetu Dar.
 

Hahahaha, mwingine huyo, jazba za nini? Yote kuwa humpendi tu Kikwete?
 
Haya halafu utuwekee pumba zako kama kawaida, lakini angalia wenzako washaanza kukushtukia maana hivi juzi juzi tu niliona wanavyoku kandia! nikasema AlhamduliLllah yale niliyoyaona mimi zamaaani wao ndio kwanza wanayaona!

Wewe Dar es Salaam -mwanakijiji ni great thinker tunamkubali humu ndani na nje ya JF -ni potential figure kwa sauti ya umma. Siyo kibaraka kama wewe harafu eti kibaraka wa makamba.
 
Good food of thought for the beggining of the year Rev. Mambo bado ni magumu sana na uongozi uliopo haata kama hautakubali, ukweli ni kuwa hauna dawa ya kutibu matatizo yaliyopo maana hawana uwezo huo.
 
Wewe Dar es Salaam -mwanakijiji ni great thinker tunamkubali humu ndani na nje ya JF -ni potential figure kwa sauti ya umma. Siyo kibaraka kama wewe harafu eti kibaraka wa makamba.

Great Tinker I agree, Great thinker? No way!
 
Nchi yetu tumeifanya nchi ya wapiga story kuanzia top most mpaka sisi watu wa chini kabisa. Lakin lawama ni kwa jamaa wa juu kupenda mdaraka wakati hawajui wakipewa madaraka watayafanyia nini!
 

Si ndio maana nika kwambia ni pumba! Mwinyi nani CCM nani? sasa fata hii link ukaone mambo ya Kikwete: https://www.jamiiforums.com/busines...ch-mortgage-financing-this-year-official.html
 
Haya halafu utuwekee pumba zako kama kawaida, lakini angalia wenzako washaanza kukushtukia maana hivi juzi juzi tu niliona wanavyoku kandia! nikasema AlhamduliLllah yale niliyoyaona mimi zamaaani wao ndio kwanza wanayaona!

tangu lini watu wanafunga safari kupanda vilima? kama huwezi kulipa gharama ya mabadiliko au misimamo yako usiiweke hadharani ujifungie chumbani tu. So wakandiaji wanakaribishwa - and you know me well to know that I can handle the punches as much as I can give mine. Its part of the same fight.
 

Kwani usharudi Tanzania to take the punches?
 

Haya ni malalamiko au mapendekezo hujaelewaka?

Unategemea kuna siku matatizo yatamalizwa kwenye nchi yeyote?

Kama ni hivyo tusingechagua wa kutoongoza kuyakabili matatizo?
 
nope na the TZ punchers are going to wait a little bit longer while I do my punches..

Wewe hauko kwenye realities (real politics) uko kwenye fantasy JF, Tanzania Daima and the like

Ukija siasa za majukwaani kwetu...you can deliver nothing
 
Na wewe majukumu yako ni pumba na fitna na chuki zisizo maana kwa Rais aliyefanya mengi mema kwa muda mfupi aliokuwepo katika uongozi kuliko ma Rais wote wa awamu zote ukijumlisha. Tutakwenda samba samba!
You keep saying rais aliyefanya mengi. Jana kule kwenye makala ya Maggid nimekuomba unipe mifano ya matatu tu makubwa aliyoyafanya Kikwete ambayo sisi Watanzania tunapaswa kujipiga vifua juu yake. Ukakimya. Umekuja huku badala ya kushambulia hoja unashambulia mtoa hoja. Haya, twende sambamba na utetezi wako wa mafisadi.
 
Rev: Your topic is certainly mind boggling.

Je, tumeweka msukumo mkubwa sana kwenye siasa kiasi cha kuamini na kuishi kwamba wanasiasa wakishindwa ndiyo hivyo tena kama nchi tumeshindwa? Hili swala la watz wengi kuanza kuamini kwamba mafanikio katika maisha hayapatikani kwa bidii isipokuwa kwa ujanja ujanja mnalionaje? Watu wanataka degree za uongo, wanajipachika ma PhD ambayo hawana, vijana wetu wanataka wafaulu hata kama hawakujiandaa kwa kusoma, wanatafuta mitihani ya kuiba badala ya kujisomea, mtu anagombea umeya huku akijia hawezi, anaongoza kwa ujanja ujanja,n.k. Je, falsafa kwamba viongozi ni kiwakilishi cha jamii husika ina-apply pia kwetu? Kwamba walivyo viongozi wetu kimsingi ndivyo na sisi wananchi wao tulivyo-kwamba tu wavivu, wapiga tanuri, wapenda maneno na misen'enyo, wababaishaji, mediocre, tunapiga vita watu wanaofanya kazi kwa bidii na wanaopenda unyoofu, tunawachukia wale wanaofuata taratibu na haki, n.k, ndivyo tulivyo kweli? Na kama ndivyo, je tunaweza kubadilika tukitaka? Na je, tuanze sisi kubadilika au tubadilishe kwanza viongozi?
 
Wote hao unaosema hawafanyi kazi vizuri wameteuliwa na rais mwenyewe. Hakuna kinachomzuia kuwafukuza na kuteua wengine. Kwa maneno mengine, ,mambo yakienda kombo wa kumlaumu ni rais mwenyewe. Hakuna mwingine zaidi. Mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na vyeo vingi sana wote wanateuliwa na rais na ndiye mwenye uwezo wa kuwaondoa kutoka kwenye nafasi hizo. Sisi wananchi wa kawaida hatuna amri wala hatuwezi kudiriki kuwaondoa. Sasa kwa nini tusimlaumu jk kwa madudu yanayoendelea hapa nchini??? Kumtetea jk ni propaganda tu. Hata wanaomtetea ukiingia mioyoni mwao utatambua kwamba nao wanaujua ukweli.
 

Kitila,

It is frustrating kuona kuwa yani kila kona tunachechemea! Ukiangalia mfano wa BoT na Hazina, hawa jamaa wawili Mkulo na Ndulu wameshindwa kabisa kubadilisha dira ya Taifa ya uchumi. Mkulo haishi kushangilia misaada na kutamba kuhusu kusambaza bakuli, huku Ndulu anashindwa kutumia maarifa yake kumwambia bosi wake "funga mkanda, punguza matumizi, punguza ukubwa wa Serikali" na alichokifanya cha maana ni kila miezi mitatu kutoa takwimu bubu na sasa katuchaopishia noti mpya ambazo zimeshaibiwa kabla hata hazijawekwa kwenye mzunguko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…