Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Usiwe mchoyo kiasi hicho.Habarini wanajukwaa!
Poleni na majukumu ya kulijenga Taifa letu pendwa Tanzania. Kuna muda nilileta ama nilikuja hapa kuomba Msaada kwa mtu anayeweza kunisaidia kwa namna yoyote nipate kazi mkono uende kinywani.
Nashukuru Kuna member mmoja alinisaidia na leo ndio siku nimepata malipo/mshahara na nimenunulia familia yangu chakula. Nashukuru mno Mungu amsaidie amnyoonyeshee njia zake zinyooke Sina Cha kumlipa zaidi ya kushukuru anayetupa pumzi ambariki zaidi na zaidi azidi kuwa na huo moyo.
Sina ama nakosa maneno ambayo naweza nikamshukuru jamani Mana nimefurahi mno na familia Leo wamefurahi mno Mana hata wamepata maziwa ya ng'ombe wa kienyeji kwa hela niliyolipwa kwa kazi hiyo aliyoniunganisha. Namie nahaaidi siwezi muangusha aje kujutia.
Wewe member popote ulipo pokea SHUKRANI zangu za dhati narudia kusema ahsante Sana na ubarikiwe wewe mkaka na hata bado sijakufahami sinakuona na simu tu imefanya kazi.
Nisiwachoshe na furaha ama SHUKRANI zangu kwa wote mlionitia moyo na kuharibu pia kunisaidia.
Pia soma: Naomba msaada wa ajira au connection
Utasemaje huna cha kumlipa?
Unaonaje umtafutie hata zawadi ndogo ya 10,000?
Mbona Waafrika wachoyo sana?
Eti sina cha kumlipa...onyesha shukrani ili hata akipata nafasi bora zaidi akukumbuke tena