Shukrani Mwanajangwani Yusuph Manji, Mafanikio yako yanaonekana.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kama mwanajangwani, ningependa kutoa shukrani na pongezi zangu binafsi kwa Mwenyekiti aliyefanikiwa kuiko mwenyekiti yeyote tuliyepaya kuwa naye Jangwani Bw Yusuph MANJI.

Mnamo jana jioni Bw Yuusph Manji aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu kwenye nafasi ya Uwenyekiti ya Mabingwa wa kihistoria wa LigiKUU Tanzania Bara kutokana na kutokutengemaa kwa Afya yake.
Mwenyekiti alieleza zaidi kuwa angependa kuachia nafasi hiyo ili apishe Mwenye nguvu zaii ya kuweza kuitumikia Yanga kwa kuwa hali yake ya kiafya hivi sasa haimwezeshi kuitumikia kikamilifu Klabu ya Mabingwa mara 27 wa kihistoria wa Tanzania.

Ningependa kuanisha baahi ya Mafanikio yake yanayoonekana kwa Macho tangu ajifungie katika mitaa ya Jangwani mnamo mwaka 2012! Kwa kipindi chote cha miaka 5. (2012 - 2017)

  1. Young Africa SC imekuwa mabingwa wa Ligi mara 4 - (2012–13, 2014–15, 2015–16, 2016/17).
  2. Young Africa SC imebeba kombe la ligi mara 1 - (2015–16)
  3. CECAFA Kagame Cup 1 - (2012)
  4. Azam Sport Fed Cup 1 - (2015/16)
JUMLA YA MAKOMBE 7 KWA MIAKA 5.


Pia tunashukuru kwa Ekari 100 ulizozikabidhi kuwa Mali ya KLABU kule kigamboni...


ZAIDI: Mafanikio ya kipekee ni kuhakikisha katika kipindi chote cha kuwa Mwk wa Mabingwa wa kihistoria Yanga SC ulihakikisha kuwa MIKIA FC hawawi Mabingwa (nakumbuka ahadi hii uliitoa mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Mwk pale Jangwani).



NK:
Kwa niaba ya wanaJangwani wote humu JamiiForum tungependa kukutakia afya njema, mkono wa mwenyezi MUNGU uwe juu yako katika kipindi hiki kigumu mpaka pale utakapo pata nafuu na kuendelee na shughui zako za kila siku.

Tunakuhaidi kuwa tutauendeleza UBABE kwenye Ligi mpaka pale Yesu atakapo rudi na kutunyakua.

Demigod - Mkereketwa Mkuu wa Mabingwa mara 27 wa kihistoria wa LIGIKUU Tanzania Bara.

 
Pia alichukua timu ikiwa kwenye mgogoro wa yanga asili vs yanga kampuni ,huu mgogoro ulikuwa hatari kipindi kile

Alivyochukua timu hali imetulia ndani ya klabu mpaka anapoondoka saizi
 
Haya mzee wa ngada. Sasa pambana na kesi zako mahakamani. Hatimaye jiondoe na udiwani. Hii bongo bwana. Hatupendagi ujinga. Kula kihalali urefu wa kamba yako. Ngada nomaaaaaaa.
 
Haya mzee wa ngada. Sasa pambana na kesi zako mahakamani. Hatimaye jiondoe na udiwani. Hii bongo bwana. Hatupendagi ujinga. Kula kihalali urefu wa kamba yako. Ngada nomaaaaaaa.
Alichowafanya hamtokuja kumpenda Kwenye siku hizi za usoni..

Maana amefanya Kabati lenu liwe tupu kwa muda sasa.[emoji23]
 
Bashite ni shabiki wa simba, alimtaja Yanga ki mkakati. Lengo ilikuwa kupoteza dira ya yanga, lkn mkakati wa bashite na simba yake mmeshindwa.

Mjipange kwa msimu ujao wa 2017/2018.
 
Hongera Yusuf M. Manji, Wapo watakaokusahau wengi watakukumbuka katika historia ya furaha upande mmoja na wengine watakukumbuka ulivyowanyima raha wakati wa Uenyekiti wako.
 
Natabiri zama za shida kunukia yanga!
 
Ukiwa Simba wewe zwazwa..Yanga wanajaza vikombe kwenye makabati...nyie mnatafuta kuifunga Yanga..ukiwa underdog kazi kweli kweli
 
Hongera Yusuf M. Manji, Wapo watakaokusahau wengi watakukumbuka katika historia ya furaha upande mmoja na wengine watakukumbuka ulivyowanyima raha wakati wa Uenyekiti wako.
 
Angerudisha TANO angekumbukwa, mtaendelea kumkumbuka Rage.

Ataruishaje 5 wakati nyinyi nio mlikuwa mnarudisha hizo tano!

Au mmesahau kuwa Juni 1, 1968 nilikupigaga bao 5? [Maulidi Dilunga kwa njia ya penalti (dk 18,43), Salehe Zimbwe (dk 54,89),Kitwana Manara (dk 86). ]
 
Pengo la Manji litazibwa na Mzee Yahaya Akili mali watani zetu Yanga Msiwe na Mushkel wala Mshawasha![emoji12][emoji12][emoji12]
 
Ukiwa Simba wewe zwazwa..Yanga wanajaza vikombe kwenye makabati...nyie mnatafuta kuifunga Yanga..ukiwa underdog kazi kweli kweli

Swali la Msingi!

Yanga inaweza kujaza Makombe bila ya Fedha za Ufadhili toka kwa Wauza na watumia Mihadarati? [emoji12] [emoji12] and
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…