Shukrani za Jamal Emil Malinzi kwa wana JF

Jamal Malinzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
710
Reaction score
650
Ndugu zangu nashukuru uchaguzi tumemaliza salama na mimi nimeshinda. Nichukue fursa hii kuwashukuru wapenzi na wadau wote wa mpira miguu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kwenye mchakato.

Siku chache zijazo nitafungua thread hapa nikiomba maoni na mapendekezo yenu kuhusu ni jinsi gani tutaimarisha timu yetu ya Taifa kwa ajili ya AFCON qualifiers Novemba mwaka ujao.

Tafadhali jiandae kuchangia.

Malinzi

Soma Dakika 90 za mahojiano na Jamal Malinzi ndani ya JF - JamiiForums
 
Jiamini,tukuamini


Hongera sana kuwa Rais wa TFF
usipageuze pango la wanyang'anyi.
 
Afanye kazi sasa,ule uwanja mzuri kwenda na furaha kurudi na.majonzi inatutesa sanaaaaaaa!!!!!!!

Ushindi sasa kwa Taifa stars nasi tufurahi!!!!!
 
safi yule mnyaa sijui mnyela imekula kwao na tenga wake, afichue ufisadi wote wa tff
 
Vp uchaguz ulikuwa huru na wa haki? ??If so,kwanini mliwatoa wahandishi wa habari nje? ?
 
Hongera sana manfesto yenu mjaribu kuyatimiza.
Zawadi kubwa ninayotarajia ni Kuiona Taifa stars wakicheza kombe la Africa na la Dunia kwa maandalizi yako mazuri 2018
 
Jihazari na matapeli wa soccar akina Aden RAGE. watu kama hao kaa nao mbali sana ni hao ndio waliiangusha soccsr ya Tanzania kutokana na ile sheria yao ya 18 ya FIFA ya timu ya nyumbani lazima ishinde wao na Ndolanga wake ndio waliotufikisha hapa tafadhari jamaa yangu JAMAL MALINZI tulikuwa tunashinda wote Kinondoni kwa Jan Fedha hao jamaa au huyom jamaa asikuzowee kabisa wacha aiuwe Simba tu
 
Kila la kheri kiongozi Mungu akutangulie utende yaliyo mema
 
Lengo halisi la kugombea Urais TFF wewe wenyewe ndiyo unalijua moyoni.
Angalizo:
1. Tumikia Taifa usileta uyanga kweny kuongoza TFF.
2. Timiza ahadi ulizo ahadi
3. Usilete ubaguzi wa aina yoyote
4. Pambana wa 'wapigaji'
 
We Jamal vipi mbona unafanya hivi,unazungukazunguka nini?!,ok.tunashukuru pia kwa shukrani zako lakini unapaswa kwenda mbaali zaidi ya hapa ikibidi tuandalie hata LUNCH kwa sababu kazi tuliyofanya ni kubwa Mno!!
 
Hongera sana Malinzi,

Tuko pamoja na tunakuunga mkono, kilichokuweka madarakani ni imani kubwa ya Watanzania kwako na ahadi zako zinazotekelezeka! Tunategemea utazitimiza, ni ukweli husiopingika kuwa hukuwa chaguo la viongozi wengi wanaomaliza madaraka yao kwa sababu zao binafsi na za kifisadi, hawa watataka kukukwamisha ili uonekane hufai kuongoza, tumia hekima, katiba na uwe mpole kama njiwa lakini mwerevu kama sungura!

Hongera sana
 
kile kiofisi chenu cha tff kinatia aibu
 
tunategemea meng mazur..hongera na kazi njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…