"Mtoto wangu Junior kawa mwanafunzi wa kwanza kati ya wanafunzi watano wanao soma darasa la pili kwenye shule ya msingi ( EMS jina kapuni)"
Hayo si maneno yangu. Ni maneno ya rafiki yangu wa " faida", Single Mother ( 26) akimzungumzia mtoto wake anae soma darasa la pili..
Ningekuwa baba wa huyo mtoto walahi huyu mwanamke angerudi nyumbani kwao na sikio moja.
Kwanini una mtesa mtoto wako kiaso hicho? Amekukosea nini?
Kwanini umpeleke mtoto wako kwenye shule kama hiyo?
A lot of Tanzanian " parents " Of now adays, have got a very little understanding about children psychology and human psychology in general.
Someni vitabu please. Someni vitabu kuhusu saikolojia ya watoto, Saikolojia ya watoto katika kujifunza.
Watoto wadogo wa shule ya msingi hawaendi shule kusomea udaktari, au Uinjinia au Uanasheria au Upilot etc.
Watoto wa shule ya msingi wanaenda shule, kucheza na Ku socialize na watoto wenzao kwa ( 80 % ) na asilimia 20 iliyo baki ndio kwa ajili ya kujifunza.
Takwa hili la asili haliwezi kutekelezeka kwenye shule ambayo darasa moja wanakaa watoto watano.
Standard ni at least kuanzia watoto 45. Hapo ndio mtoto anaweza kufurahia utoto wake ( Childhood) to the fullest.
Kwa sababu watoto wana kuwa ni wengi na michezo inakuwa mingi.
Mtoto anatakiwa kuwa kwenye darasa ambalo mwalimu akisema, " Watoto sema A" , sauti zilizo changamka, zenye afya na bashasha, zinaitikia " A". Jambo hilo lina tengeneza a very powerful Psychological effect to the brain of a child who is in that class.
Hiyo positive energy inayo tengenezwa kwenye atmosphere yenye watoto arobaini na tano au zaidi ndani ya darasa moja ni muhimu Sana kwenye ubongo na nafsi ya mtoto. Kitu hicho hawezi kukipata kwenye darasa lenye wanafunzi wa tano.
Sana Sana effect atakayo ipata kwenye darasa lenye wanafunzi watano ni sonona na upweke wa hali ya juu Sana jambo ambalo litalemaza hata akili yake na kumuathiri mtoto ki saikolojia in a very long time basis, na atakuwa nalo, kwa sababu ubongo wa mtoto mdogo haujawaha biologically wired kuwa katika atmosphere yenye upweke kiasi hicho.
Darasa moja watoto watano, huyo mtoto si atakuwa bored to the fullest.
Watoto watano. Wasichana wangapi wavulana wangapi?
Siku mmoja akiumwa wana kuwa wanne, mmoja akihamishwa wana kuwa watatu. Au hao wanne. " WAKIMGAYA" mtoto wako ana kuwa hana wa kucheza nae siku hiyo upweke juu ya upweke.
Uwepo wa watoto wengi wa kucheza pamoja ni jambo linalo mmotivate mtoto kupenda shule kwa kiasi kikubwa Sana.
Kumtupa mtoto wako kwenye darasa lenye wanafunzi watano tu ni kumfanyia ukatili " Child abuse" Wa kiwango cha juu mno, na hakika, gharama utakuja kuzilipa baadae kwa sababu akisha fikia kwenye rebellious age, ubongo wake utatafuta kitu cha kucompasate na hilo takwa la kisaikolojia alilolikosa utotoni, so atajiunga na timu ya mpira wa miguu mtaani, huko atajifunza kuvuta bangi etc ili aendane na wenzake.
Eti unaogopa mtoto wako asikae kwenye shule yenye watoto wengi kwa sababu unaogopa mtoto wako kukutana na pilika pilika na kelele/ fujo za watoto wenzake .. Nani alikwambia mtoto mdogo hapendi kelele na mikiki mikiki ya watoto wenzake?
Kiuhalisia, ubongo wa mtoto mdogo ndio unazifurahia hizo kelele na hizo pilika pilika na watoto wenzake.
Hivi mkiwapeleka watoto wenu kwenye mabembea wakati wa likizo hamuonagi wanavyo enjoy kumingle na watoto wenzao wengi.
Kwa sababu wewe hupendi kelele kwa sababu ya madeni ya vikoba, basi una assume mtoto wako nae hapendi kelele na pilika pilika za watoto wenzake.
Watoto wana enjoy zaidi hizo kelele za watoto wenzao kuliko unavyo weza kufikiri.
As a matter of fact, hata watu wazima tuna enjoy sehemu zinazo happen, zenye watu wengi.
Nitaenda kwenye bar yenye watu wengi.
Mpirani uta enjoy kama uwanja umejaa etc.
Hata msiba ukiwa na watu wengi ndio wafiwa wanafarijika.
Binadamu anatakiwa kuishi maisha yake to the fullest.
Nyakati pekee inayo weza Ku guarantee jambo hilo ni his childhood.
Muache mtoto wako aishi maisha yake to the fullest.
Pengine ndio kipindi pekee atakacho yafurahia maisha yake to the fullest.
Sisemi umpeleke mtoto wako Kayumba ili akafurahie maisha yake ya utoto to the fullest( kwa sababu ukweli ndio huo), ila nasema mtafutie mtoto wako shule hiyo hiyo ya EMS unayo itaka wewe ambayo ina wanafunzi at least 45 kill darasa.
KINGINE: Mtoto wa darasa la kwanza na la pili anatakiwa kukaa darasani kwa masaa manne tu na sio masaa kumi na mbili.
Mnaukumbuka wimbo wa enzi zetu " Wa saa nne makombo, wa asubuhi oye oye "
Darasa la pili hilo wiki ya kwanza MNA kuwa wa asubuhi mnaenda shule sa moja mnatoka saa nne then wenzenu wanaingia sa nne wanatoka saa nane. ( Those were the days)