Shule kongwe 84 zimefanyiwa ukarabati na Serikali Nchini

Shule kongwe 84 zimefanyiwa ukarabati na Serikali Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SHULE KONGWE 84 ZIMEFANYIWA UKARABATI NA SERIKALI HAPA NCHINI

Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa ameuliza swali Wizara ya TAMISEMI kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Rungwe, Anthony Albert Mwantona

"Taratibu za kutekeleza agizo lililotolewa na Waziri Mkuu la kukarabati Shule ya Sekondari Kayuki zinaendelea ambapo Halmashauri imekamilisha BOQ kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Kayuki na imebainika kuwa Shilingi Milioni 776 zinahitajika" - Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

""Utaratibu kwa ajili ya kupata fedha za kukarabati Shule ya Sekondari Kayuki unaendelea ambapo ukarabati mdogo kwenye hosteli na Jengo la Utawala umefanyika kwa Shilingi Milioni 17.4. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ukarabati" - Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Mkoa wa Mbeya kuna Shule nyingi kongwe ambazo zimechakaa sana zinahitaji ukarabati mkubwa. Lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Shule Mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla? - Mhe. Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Wilaya ya Chunya kuna Shule kongwe ambazo zipo tangu enzi za mkoloni lakini Serikali ilesema itatoa fedha kwa ajili ya ukarabati, Je, lini Serikali itatoa fedha ili ukarabati uweze kufanyika? - Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa

"Rais Samia alitafuta fedha kwaajili ya ukarabati wa Shule Kongwe na tayari Shule Kongwe 84 hapa nchini zimekwisha karabatiwa ikiwemo zilizopo Mkoa wa Mbeya. Serikali itaendelea kutafuta fedha kwaajili ya kuendelea na ukarabati wa Shule kongwe hapa nchini" - Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Shule kongwe kwa Wilaya ya Chunya tutaangalia katika awamu inayofuata ya ukarabati wa Shule kongwe tuweze kuweka kipaumbele vilevile kwenye shule kongwe Wilaya ya Chunya" - Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI.

WhatsApp Image 2023-06-06 at 18.13.26.jpeg
maxresdefaultkio.jpg
Screenshot_20230530-183056.png

 
Back
Top Bottom