Pre GE2025 Shule mpya 71 zajengwa Geita miaka minne ya Rais Samia

Pre GE2025 Shule mpya 71 zajengwa Geita miaka minne ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Serikali imejenga shule mpya 171 na vyumba vya madarasa 3,300 kwa Mkoa wa Geita kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan lengo likiwa kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta elimu.

1740899126388.png
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigella, ameyasema hayo wakati akipokea vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa na kampuni ya Usafirishaji ya BlueCoast katika shule ya Msingi Bombambili katika Manispaa ya Geita.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema kinachofanywa na wadau wa maendeleo kujenga shule ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha elimu inapatikana katika mazingira bora na rafiki.

"Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Samia Mkoa umejenga shule mpya 171 tunazo za Msingi ziko 90 na Sekondari 81 Mzee Inyasi unapopata fedha na kuamua kufanya jambo kama hili ujue unamuunga mkono Rais Samia kuleta maendeleo" - amesema Shigella.

CHANZO: Nipashe
 
Pamoja na ''kujenga'' shule zote hizi, pamoja na ''maendeleo'' yote anayoleta, na fedha anazotoa kila sehemu ya Tanzania, lakini bado anaogopa majina ya wapinzani kuwa kwenye karatasi za kura wakati wa uchaguzi.
 
Duu shule 171 huo mkoa ulikua hauna shule ata moja kwamiaka yote mpaka alipoongozza mama.uzuri iliokua inatawala na inaendelea kulawala ni ccm.hongeren wanageita.kura kwa mama
 
Back
Top Bottom