Angalizo kwa wote ambao mna bado watoto watakaojiunga sekondari o-level ni kwamba shule nzuri interview zake ni kati ya August - October ila nyingi September. Form za shule hizi zinaanza kutoka kuanzia July na chache sana hadi September. Shule hizi mara nyingini zile top 10, 20, 30, 40, 50!!!!! katika school ranking. Na mwanao ili azipate kichwa kiwe kinachemka hasa maths, Science, general knowledge na English. Form nyingi zinapatikana Msimbazu Centre kwa DSM ila ukienda pale uwe tayari imeshapitia mtandao na kuchagua shule zinazofaulu ili usibabaike maana pale msimbazi hata zile shule za mikia form zipo. Kwa sasa huwezi kupata form za Marian, Canossa, St. Joseph, Anwarite, Mary Goreth etc. Kwa uhakika kama uko Dar nenda Msimbazi Centre. Mitihani ya zile top schools tayari imefanyika na inaendelea......