Shule Nzuri Private, Girls & Boarding ya Form 1

Shule Nzuri Private, Girls & Boarding ya Form 1

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Wadau wa hili jukwaa,

Mchango wenu wa mawazo unahitajika. Mtoto wangu wa kike amemaliza STD 7 last 2 weeks hivyo namtafutia Boarding, girls, private na iwe mkoani ili kupunguza unnecessary likizo.

Iwe inayotoa matokeo mazuri na yenye maadili. Na isiwe expensive sana.

Mwenye kuijua shule ya hivi msaada please qq
 
Wadau wa hili jukwaa,

Mchango wenu wa mawazo unahitajika. Mtoto wangu wa kike amemaliza STD 7 last 2 weeks hivyo namtafutia Boarding, girls, private na iwe mkoani ili kupunguza unnecessary likizo.

Iwe inayotoa matokeo mazuri na yenye maadili. Na isiwe expensive sana.

Mwenye kuijua shule ya hivi msaada please qq

Ni pm nikupe shule nzuri kaka...
..
 
St Frances ipo mbeya. Ada ni 1,990,000 kwa mwaka. Na imeongoza miaka 4 mfululizo.
 
st.christina nishule yakawaida sana siku hizi....naijua vizuri hii shule.....

nimesoma same iliyokua ya 4 mwishoni kimkoa lakini kuna one 12 na yangu nimojawapo,,,ye anataka shule zisizo na gharama kubwa,,kandoto wako poa nikiwa form v walikua wa11 kitaifa, st.christina wanafundisha vizuri ufaulu ni vichwa vya wanafunzi na unatofautiana mwaka hadi mwaka,nashkuru
 
Shule ya visitation girls iliyopo mkoa wa kilimanjaro ndani ya wilaya ya siha ni nzuri sana hasa kwa kuanza kidato cha kwanza.
 
Shule nzuri private halafu isiwe na gharama kubwa! - Hapo kuna mgongano!
 
Kama mfuko wako uko vizuri, na mwanao akili zinachaji, Marian Girls ni mahala sahihi kwake.
 
Shule ya visitation girls iliyopo mkoa wa kilimanjaro ndani ya wilaya ya siha ni nzuri sana hasa kwa kuanza kidato cha kwanza.

Mkuu hiyo visitation ni ya mission? kama ndiyo shirika gani wanamiliki? ilishafaulisha form four? Kama ndiyo rank yaje kitaifa ni vipi?
 
Angalizo kwa wote ambao mna bado watoto watakaojiunga sekondari o-level ni kwamba shule nzuri interview zake ni kati ya August - October ila nyingi September. Form za shule hizi zinaanza kutoka kuanzia July na chache sana hadi September. Shule hizi mara nyingini zile top 10, 20, 30, 40, 50!!!!! katika school ranking. Na mwanao ili azipate kichwa kiwe kinachemka hasa maths, Science, general knowledge na English. Form nyingi zinapatikana Msimbazu Centre kwa DSM ila ukienda pale uwe tayari imeshapitia mtandao na kuchagua shule zinazofaulu ili usibabaike maana pale msimbazi hata zile shule za mikia form zipo. Kwa sasa huwezi kupata form za Marian, Canossa, St. Joseph, Anwarite, Mary Goreth etc. Kwa uhakika kama uko Dar nenda Msimbazi Centre. Mitihani ya zile top schools tayari imefanyika na inaendelea......
 
Agape lutheran junior seminary ipo mosh form znapatkana azania front
 
usimpeleke girls tupu atajifunza ulesbian...kuna rafiki yangu amesoma shule hizo ni lesbian wa kufa mtu..bora boyz n girlz kidogo
 
mkuu hiyo visitation ni ya mission? Kama ndiyo shirika gani wanamiliki? Ilishafaulisha form four? Kama ndiyo rank yaje kitaifa ni vipi?

iko chini ya shirika la masister wa kanisa katoliki kilimanjaro,ufaulu wake hasa kwa o level uko juu sana
 
Back
Top Bottom