chuwaalbert
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 3,598
- 2,118
Asante kwa historia NZURI. Naomba kunyoosha historia, hasa sehemu nilizoweka rangi.MWAKA 1848, Mmishenari wa Kijerumani Dk Johan Ludwig Krapf, alitembelea kijiji cha Magila kilichopo Muheza mkoani Tanga akiwa katika safari zake za Afrika Mashariki.
Dk Krapf alipofika na kuwaona wagonjwa hao waliokuwa wakiishi kwa madhila makubwa, alichonga msalaba katika mti wa mkuyu kwa imani kuwa Mwenyezi Mungu angewaponya wagonjwa hao.
Eneo hilo ndilo lililokuja kujengwa shule ya kwanza na Waingereza mwaka 1886. Alama ya msalaba huo ipo hadi na sasa na ndipo ilipo Shule ya Sekondari Hegongo.
Hadi leo mahali hapo panaitwa Magila Msalabani. Kwa sasa Magila ni kata yenye vijiji vya vya Magila, Mikwamba, Misongeni na Mafleta.
Anawataja baadhi ya Wamishenari hao kuwa ni pamoja na David Livingstone, Charles Mackenzie, William Tozer na Edward Steer.
Anasema harakati hizo zilianzia tangu visiwa vya Zanzibar mwaka 1863 ambako pia walikomesha biashara ya utumwa na kuanza ujenzi wa kanisa la Anglikana la Mkunazini Zanzibar kwa miaka 10 tangu mwaka 1873.
Anasema wakati huo kulikuwa na shule iliyoanzishwa Zanzibar maeneo ya Kiungani na Kiinua mguu na Askofu William Tozer mwaka 1869. Hata hivyo, anasema shule hiyo haikuwa rasmi na ilikuwa ikifundisha elimu ya dini kwa watumwa waliokombolewa.
Uamuzi wa kujenga shule Bara
Mnamo Agosti 13, 1967 Askofu Tozer alimtuma Padri CA Alington aende Vuga (Lushoto) kwa Chifu Kimweri ili apate kibali cha kujenga kituo cha misheni kwenye maeneo ya Bara,anasimulia Luteni Kanali Mhina na kuongeza:
Baadaye Januari 20, 1868, Padri Alington alirudi Vuga na kuruhusiwa na Chifu Kimweri kujenga sehemu yoyote katika maeneo ya Pwani.
Anasema Padri Alington aliamua kuchagua eneo la Magila ambalo lilikwishajulikana kutokana na alama ya msalaba uliowekwa na Dk Krapf.
Shule ya sokoni ilikuwa kwanza kujengwa maeneo hayo mwezi Aprili 1869 chini ya Padri Fraser na wanafunzi wake walikuwa ni pamoja na Jumbe Kifungiwe na ndugu yake Sagosago na vijana wengine. Palikuwa na soko dogo na mti mkubwa wa Mzindanguuwe, watu wazima walipenda kukaa hapo ili walione jambo hilo geni, anaongeza kusema.
Sekondari ya Hegongo
Hivi sasa eneo hilo kuna shule iitwayo Hegongo. Mkuu wa shule hiyo, Wilfred Mdimu anasisitiza kuwa eneo hilo ndipo palipojengwa shule ya kwanza Tanzania ambapo mpaka sasa kuna mabaki ya darasa la kwanza lililojengwa na Wamisheni.
Hivi sasa anasema darasa hilo linatumiwa kama ofisi ya walimu wa shule ya sekondari ya kata Magila.
Hili ndilo darasa la kwanza lililojengwa mwaka 1869 na Waingereza. Awali lilikuwa ghorofa lakini likabadilishwa. Inasemekana shule nyingine ilijengwa Bagamoyo na baadaye Minaki, anasema Mdimu na kuongeza,
Mwaka 1974 hadi 75, majengo hayo yakafanywa kuwa mahali pa kujifungulia wanawake na ndipo ilipoanzia hospitali teule ya Muheza. Lakini ikahamishiwa eneo ilipo sasa na majengo haya yakabaki matupu, anasema Mdimu.
Kuanzishwa kwa Hegongo sekondari
Mwalimu Mdimu anasema baada ya majengo kubaki matupu, mwaka 1976 wenyeji wa Magila walimwomba Askofu wa kanisa hilo dayosisi ya kaskazini John Ramadhani, ili waanzishe shule ya sekondari hasa kwenye majengo ulipo msalaba wa Dk Krapf, naye akawakubalia.
Februari 24, 1977 shule ya Hegongo ilianzishwa ikiwa chini ya wenyeji wa Magila ili kuwapa elimu watoto wa wilaya hiyo, anasema.
Hata hivyo anasema shule hiyo haikuwa na maendeleo mazuri kwa muda mrefu. Isitoshe, wasimamizi wa shule hiyo walishindwa kuiendesha kutokana na madeni makubwa ya umeme, mishahara ya watumishi na mafao yao.
Hegongo ya sasa
Anasema hadi mwaka 2000 wasimamizi wa shule hii walishindwa kabisa kuiendesha wakairudisha kwa kanisa.
Tangu wakati huo uongozi wa kanisa umeamua kuiendesha kwa kwa kulipa madeni makubwa yaliyokuwepo na kuimarisha hali ya elimu, anasema na kuongeza:
Kwa upande mwingine, majengo ya zilizokuwa shule za St. Marys na St. Martin sasa zimechukuliwa na Serikali, huku mojawapo ikitumika kama shule ya sekondari ya kata ya Magila na nyingine kama shule ya msingi.
Mwananchi
1. 1967, ilikuwa 1867.
2. Askofu John Ramadhani (wakati huo) alikuwa wa Dayosisi ya Zanzibar na Tanga, (siyo Dayosisi ya kaskazini. Hapa mwandishi, pengine, kachukua mfumo wa KKKT. Kwa sasa Dayosisi hiyo ya Anglikana, imegawanywa kuwa dayosisi mbili: Dayosisi ya Zanzibar na Dayosisi ya Tanga.
3.Hapo kwa Dkt. Livingstone, yeye alishughulika zaidi na Umisioni Afrika ya Kati. Ripoti yake ndio iliyoibua hamasa kwa wanafunzi na wana taaluma wa Vyuo Vikuu vya Oxford na Cambridge kujiunga na Mision ya UMCA (University Mission for Central Africa) kwenda kupeleka ijnili "Afrika ya kati". Wakilenga zaidi Malawi, Zambia na Zimbabwe.
Kutokana na kushindwa kuingia eneo hilo kupitia Afrika ya Kusini, Walitumia Zanzibar. Shirika lao ni la Kiangilikana (lenye mlengo wa Ki Katoliki. Wao wanauita High Church.Ndio maana wanawaita Makasisi wao "Padri"). Maaskofu wake 3 wa kwanza ni Charles Mackenzie, William Tozer na Dkt. Edward Steer. Walieneza Injili kwa Kaskazini hadi Magila (baadae Korogwe). Hapa ndipo yalipo Makao Makuu ya Dayosisi ya Tanga. Walienea pia Dar es Salaam, Masasi, Ruvuma, Njombe na Mbeya.
Eneo hili ndilo limetoa Dayosisi za Anglikana zenye mfumo wa "High Church" za zanzibar, Tanga, Dar es Salaam, Masasi, Newala, Ruvuma, South Western Tanganyika (Njombe) na Sourthern Highlands (Mbeya).
Kwa taarifa, Dayosisi nyingine za Kanisa hilo zinafuata mfumo wa "Low Church" na zinatokana na shirika la Kimissioni la Church Mission Society (yaani CMS). Hawa wana historia tofauti kidogo. Hii ilianza na Dayosisi ya Central Tanganyika (Mwaka 1927). Hapa ndipo yalipo Makao Makuu ya Kanisa hilo Nchini.