Shule ya kwanza Tanganyika ilijengwa na waingereza huko Muheza

Asante kwa historia NZURI. Naomba kunyoosha historia, hasa sehemu nilizoweka rangi.
1. 1967, ilikuwa 1867.
2. Askofu John Ramadhani (wakati huo) alikuwa wa Dayosisi ya Zanzibar na Tanga, (siyo Dayosisi ya kaskazini. Hapa mwandishi, pengine, kachukua mfumo wa KKKT. Kwa sasa Dayosisi hiyo ya Anglikana, imegawanywa kuwa dayosisi mbili: Dayosisi ya Zanzibar na Dayosisi ya Tanga.
3.Hapo kwa Dkt. Livingstone, yeye alishughulika zaidi na Umisioni Afrika ya Kati. Ripoti yake ndio iliyoibua hamasa kwa wanafunzi na wana taaluma wa Vyuo Vikuu vya Oxford na Cambridge kujiunga na Mision ya UMCA (University Mission for Central Africa) kwenda kupeleka ijnili "Afrika ya kati". Wakilenga zaidi Malawi, Zambia na Zimbabwe.
Kutokana na kushindwa kuingia eneo hilo kupitia Afrika ya Kusini, Walitumia Zanzibar. Shirika lao ni la Kiangilikana (lenye mlengo wa Ki Katoliki. Wao wanauita High Church.Ndio maana wanawaita Makasisi wao "Padri"). Maaskofu wake 3 wa kwanza ni Charles Mackenzie, William Tozer na Dkt. Edward Steer. Walieneza Injili kwa Kaskazini hadi Magila (baadae Korogwe). Hapa ndipo yalipo Makao Makuu ya Dayosisi ya Tanga. Walienea pia Dar es Salaam, Masasi, Ruvuma, Njombe na Mbeya.
Eneo hili ndilo limetoa Dayosisi za Anglikana zenye mfumo wa "High Church" za zanzibar, Tanga, Dar es Salaam, Masasi, Newala, Ruvuma, South Western Tanganyika (Njombe) na Sourthern Highlands (Mbeya).
Kwa taarifa, Dayosisi nyingine za Kanisa hilo zinafuata mfumo wa "Low Church" na zinatokana na shirika la Kimissioni la Church Mission Society (yaani CMS). Hawa wana historia tofauti kidogo. Hii ilianza na Dayosisi ya Central Tanganyika (Mwaka 1927). Hapa ndipo yalipo Makao Makuu ya Kanisa hilo Nchini.
 
mkuu shule ilijengwa na Waingereza au Wajerumani?
Ilijengwa na WAINGEREZA (wa Kanisa Anglikana), pamoja na kuwa wakati huo "Watawala" walikuwa Wajerumani. Wajerumani walikuja na Ulutheri.
Miongoni mwa shule walizojenga eneo hilo (ambalo kwa sasa kwa KKKT ni Dayosisi ya Kaskazini Mashariki-chini ya Askofu Dkt. Munga, ni Lwandai. Shule hii, ilihamishiwa Ilboru mwaka 1946. infact ndio iliyo "zaa" Ilboru Sekondari tuijuayo sasa. Hapa wamesoma watu wengi tu miongoni mwao Fred Sumaye, Paskali Mayalla, Hayati Sengondo Mvungi, wabunge 4 wa sasa wa Mkoa wa Singida: Allan Kiula, Antipasi Mnghway (Tundu Lissu), Lazaro Nyalandu na Mwigulu Nchemba...Miongoni mwa wengi.
Lwandai pia ndiyo chimbuko la Magamba Sekondari, mahali ambapo kipo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (yaani SeKoMU)....
 
Daah huyo mhina ni babu yangu kafsriki mwezi mmoja sasa tumemzikA magila masoroko.
 
Makala nzuri,ila ingependeza zaidi kama kungekuwa na picha za kutosha.
 
kaka miongoni mwa shule walizojenga wakati huo ni w3ajerumani au waingereza?kwa kumbukumbu sikumbuki mwaka wajerumani walijenga shule za msingi za kuishia darasa la nne na lengo kupata makarani kwa wakati wao sikumbuki mwaka ila nikipita hicho kitabu nitakiweka na picha ya hiyo shule na kinasema shule ya kwanza tanganyika ya wajerumani ilikua vuga huku usambara.
kuhusu lwandai ni ya kkkt dayosisis ya kaskazini mashariki ila ninavyojua mashirika yalitoleta injili tanga na kilimanjaro na arusha ni tofauti.
nakubali kukosolewa mkuu nipe ufafanuzi
 
mkuu miaka naona kwenye miaka kuna walakini mfano mwaka 1967 siamini ndo mwaka walioamua kuamia bara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…