Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Shule ya Meta Sekondari ambayo miaka kadhaa kabla ya Uhuru ilijulikana kwa jina la N. A. Middle School, ni moja ya shule za boding'i za wavulana tu na baada ya Uhuru ikajumuisha na wasichana wasiolala shuleni.
Mji wa mbeya ulikuwa na shule za tatu kati(middle) tatu, yaani N.A. wavulana, Meta wasichana, hii ilikuwa imechanganywa na Loleza Sekondari ambapo robo ya kwanza miaka ya sitini ilihamishiwa eneo la Foresti karibu na gereza la Luanda, na baadae Mbata mchanganyiko.
Ilipofika miaka ya themanini CCM ikaichukua shule ya N.A. Middle School ambayo ilitoa wakurugenzi wengi serikalini na mashirika ya umma na kuifanya mali yake! Katika hali ya kawaida, hatutegemei serikali kushindwa kuendesha shule na kuishia kuiuza kimyakimya, ni vizuri serikali ieleze ni vipi iliipa CCM hiyo shule ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya uendeshaji tangu ilipochukuliwa.
Ushauri, ni vizuri serikali iichukue hiyo shule badala ya kuipa pesa za kuiendesha kinyume na sheria kama ambavyo ilivyoipa CCM pesa za kuvifanyia matengenezo viwanja vya mpira vilivyokuwa mali ya serikali.