KERO Shule ya Msingi Mbosho Wilaya ya Hai, shule ni mbovu kiukweli ina ufa kila sehemu inavuja maji ndani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Shule ya Msingi Mbosho, Iliyopo Kata Ya Masama Kati, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.

Hii shule ni mbovu kiukweli ina ufa kila sehemu inavuja maji ndani. Naomba mtusaidie kwa hili.

Shule Ya Msingi Mbosho iliyopo kata ya Masama Kati Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro nimiongoni mwa Shule kongwe zilizopo Wilayani Hai, Kwa Sasa Shule hii Inakabiliwa na Uchakavu Mkubwa wa majengo ya Madarasa na Ofisi ya Waalimu.

photo_2025-12-28_18-02-28.jpg
photo_2025-12-28_17-11-12.jpg

Shule hii kwa Sasa Ukiitembelea Hali yake inatisha, Majengo yakiwa katika Hali mbya ya Uchakavu Mkubwa , Uchache wa Madarasa na ubovu wa Miundombinu kwa Ujumla.

Wananchi wanadai kuwa Majengo Mengine ya Shule hiyo yalibomoka kutokana na Kuchakaa Hali iliyosababisha Shule hiyo kubaki na Majengo manne tu ya Madarasa.

Pichani Ni Jengo la Darasa La kusomea wanafunzi katika Shule Ya Msingi Mbosho iliyopo kata ya Masama Kati Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

photo_2025-12-28_18-02-39.jpg

Shule ya Msingi Mbosho Ni Miongoni mwa Shule inayokabiliwa na Uchakavu Mkubwa wa Majengo ya Madarasa ya kusomea Wanafunzi.

Baadhi Ya Wananchi wa Kijiji Cha Mbosho Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameeleza kuwa Kutokana na Uchakavu Mkubwa wa Shule ya Kijiji Hicho Shule ya Msingi Mbosho, wanalazimika Kuwahamisha watoto wao katika Shule hiyo na kuwapeleka katika Shule za vijiji vingine Vya Mroma na Vijiji vya Jirani.

Kutokana na Hali hiyo ya Uchakavu, Wananchi wanadai kwa kiwango kikubwa wanafunzi wengi wamehamishwa katika Shule hiyo na Kwasasa Shule hiyo inaidadi ya Wanafunzi wasiozidi 100 Hali inayoashiria kuwa Shule hii huenda ikaenda kufa siku si nyingi.

photo_2025-12-28_17-19-35.jpg
photo_2025-12-28_17-16-37.jpg
 
Attachments

  • photo_2025-12-28_17-11-18.jpg
    photo_2025-12-28_17-11-18.jpg
    312.3 KB · Views: 34
  • photo_2025-12-28_17-11-14.jpg
    photo_2025-12-28_17-11-14.jpg
    261.5 KB · Views: 39
Shule ya Msingi Mbosho, Iliyopo Kata Ya Masama Kati, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.

Hii shule ni mbovu kiukweli ina ufa kila sehemu inavuja maji ndani. Naomba mtusaidie kwa hili.

Shule Ya Msingi Mbosho iliyopo kata ya Masama Kati Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro nimiongoni mwa Shule kongwe zilizopo Wilayani Hai, Kwa Sasa Shule hii Inakabiliwa na Uchakavu Mkubwa wa majengo ya Madarasa na Ofisi ya Waalimu.

Shule hii kwa Sasa Ukiitembelea Hali yake inatisha, Majengo yakiwa katika Hali mbya ya Uchakavu Mkubwa , Uchache wa Madarasa na ubovu wa Miundombinu kwa Ujumla.

Wananchi wanadai kuwa Majengo Mengine ya Shule hiyo yalibomoka kutokana na Kuchakaa Hali iliyosababisha Shule hiyo kubaki na Majengo manne tu ya Madarasa.

Pichani Ni Jengo la Darasa La kusomea wanafunzi katika Shule Ya Msingi Mbosho iliyopo kata ya Masama Kati Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

View attachment 3521830

Shule ya Msingi Mbosho Ni Miongoni mwa Shule inayokabiliwa na Uchakavu Mkubwa wa Majengo ya Madarasa ya kusomea Wanafunzi.

Baadhi Ya Wananchi wa Kijiji Cha Mbosho Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameeleza kuwa Kutokana na Uchakavu Mkubwa wa Shule ya Kijiji Hicho Shule ya Msingi Mbosho, wanalazimika Kuwahamisha watoto wao katika Shule hiyo na kuwapeleka katika Shule za vijiji vingine Vya Mroma na Vijiji vya Jirani.

Kutokana na Hali hiyo ya Uchakavu, Wananchi wanadai kwa kiwango kikubwa wanafunzi wengi wamehamishwa katika Shule hiyo na Kwasasa Shule hiyo inaidadi ya Wanafunzi wasiozidi 100 Hali inayoashiria kuwa Shule hii huenda ikaenda kufa siku si nyingi.

View attachment 3521828View attachment 3521829
Kafie mbele
 
Back
Top Bottom