Shule ya Sekondari ina wanafunzi wawili tu kidato cha tatu

Shule ya Sekondari ina wanafunzi wawili tu kidato cha tatu

dedam

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
845
Reaction score
166
Shule ya sekondari kizomla iliyoko kata ya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ina wanafunzi wawili tu wa kidato cha tatu.

Shule hiyi iliyoko umbali wa takribani km 80 hivi kutoka mkoa wa Dar es Salaam imewapata wanafunzi hao baada ya wengine kufeli kidato cha pili katika mtihani uliyofanyika nchini kote mwaka 2012

Wanafunzi hao pekee ambao ni mapacha wa jinsi ya ke ndio wanaibeba shule kwa kidato cha tatu.
 
Licha ya udhaifu wa serikali ya CCM kwenye sekta ya elimu kwa hayo maeneo ya Pwani kuna matatizo ya desturi hasi za jamii kwenye elimu, ndoa za utotoni na wazazi kujitenga kwenye kusimamia na kuendeleza elimu ya watoto wao ni mdogo. Hata top ten ya shule zilizofanya vibaya CSEE 2012/2013 ni shule toka mikoa ya Pwani,Dar es salaam,Tanga,Lindi na Mtwara. Ukweli ni mchungu ila unaponya!
 
Wanafunzi wawili mwalimu mmoja.
Good!!
Naomba nitumie maneno yako katika 'utafiti' wangu ili kuonyesha kuwa kwa wale wanaochaguliwa kuingia elimu ya juu kuna upendeleo.

Stats zinaonyesha kuwa maeneo yenye ratio ya wanafunzi kwa walimu 25:1 wanaochaguliwa university ni wengi kuliko maeneo yenye ratio ya 2:1 kama mkuranga(international standard)

Katika utafiti wangu nitaonyesha kuwa waliomaliza form 4 kuingia form 5 ni kidogo sana hata kama mkuranga ina wakazi wengi kuliko kule Magila.

Kwamba NECTA imefelisha kidato cha 2 hata kama wanafunzi hao wamekuwa wanafundisha wenzao mitaani.

Source ya data sitaweza kuweka hapa wanajamvi.

Tuna mengi ya kuwaeleza, mlikuwa mnajua historia ya mkuranga kuwa darsa lenye wanafunzi 2.
 
Shule ya sekondari kizomla iliyoko kata ya mkamba wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani,ina wanafunzi wawili tu wa kidato cha tatu,Shule hiyi iliyoko umbali wa takribani km 80 hivi kutoka mkoa wa Dar es Salaam imewapata wanafunzi hao baada ya wengine kufeli kidato cha pili,mtihani uliyofanyika nchini kote mwaka 2012, wanafunzi hao pekee ambao ni mapacha wa jinsi ya ke ndio wanaibeba shule kwa kidato cha tatu.

Safi TANZANIA, Unajengwa na wenye moyo unaliwa na wajanja.
 
Ah! Nanren ndugu yangu mbona unanisukumia zogo? Mi nilishawahi kuongea nikaambiwa nilete ushahidi. Nikatoa ule wa Kilwa nikaambiwa mzushi, kigagula,domobovu,mpayukaji n.k
Mwenyezi mungu ana heri na rehema zake hata uzi ule kabla haujakauka Mola kaleta ushahidi.

Hili neno zito naona niwasukumie wengine wenzangu

cc Mag3, Jasusi, Wickama, JokaKuu

Haki ya Mungu iko Kazi; Nanren unataka Ritz anirushie makonde!!!!!! hebu chunguza hao mapacha ni dini gani usijekuta ni wasabato (hahahahahaha). Nilisema hiki kitu kuwa lushoto ni waislamu lakini wanagangamara nikarushiwa aya ili nikae kimya haya sasa angalia.

cc Ritz, Mohammed Said, Prishaz (just in case of emergency), Kadogoo, BigShow
 
Kwamba NECTA imefelisha kidato cha 2 hata kama wanafunzi hao wamekuwa wanafundisha wenzao mitaani.

Mkuu naomba utambue kuwa NECTA haihusiki na Mtihani wa Kidato cha Pili mtihani huo unatungwa na kusahihishwa na Wizara. Hivyo naomba kauli yako isomeke:

"kwamba Wizara mefelisha Kidato cha 2 hata kama wanasunzi wamekuwa wanafundisha wenzao mitaani
 
wale vijana wanafunz wa shule ya sekondari kizomla mwaka huu ndio wapo kidato cha nne na ni wanafunzi pekee wanaunda kidato cha nne wameongzek wamefka watatu mungu awatangulie wafaulu
 
Hakuna udini unaochochewa hapo hiyo ni hali halisi ya shule zetu kwa ujumla shule hii ni majanga serikal imejenga hostel sas wanafunzi watatoka wapi wa kukaa hostel hizo
 
Back
Top Bottom