KERO Responded Shule ya Sekondari Kipande, Wilayani Nkasi - Rukwa haina madawati, Wanafunzi wanakaa chini

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest

Nkasi.jpg

Licha ya jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia nchini, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipande iliyopo Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa Wanafunzi wanaendelea kusoma katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa madawati.

Shule hiyo ilianzishwa Mwaka 2006 na inatoa elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne. Hata hivyo, zaidi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, changamoto ya ukosefu wa madawati bado haijapatiwa ufumbuzi.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hulazimika kukaa chini wakati wa vipindi darasani. Mazingira hayo si tu kwamba yanapunguza utulivu wa kujifunza, bali pia yanaweza kuathiri umakini, afya na matokeo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Wananchi na wadau wa elimu wanaeleza kuwa ni vigumu kufikia malengo ya kuboresha ubora wa elimu wakati wanafunzi wanalazimika kusomea sakafuni kwa kukosa samani za msingi kama madawati.

Wito kwa mamlaka husika, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kufanya tathmini ya haraka ya mahitaji ya shule hiyo na kuhakikisha inapata madawati ya kutosha ili wanafunzi wapate mazingira salama na yenye staha ya kujifunzia.

Elimu bora huanza na mazingira bora ya kujifunzia. Kukosekana kwa madawati katika shule iliyodumu kwa takribani miongo miwili ni changamoto inayostahili kushughulikiwa kwa haraka ili wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipande wapate haki yao ya msingi ya kusoma katika mazingira yanayowezesha kujifunza kwa ufanisi.

Ufafanuzi wa Halmashauri ~ Nkasi DC: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipande hawakai chini, hata hivyo tutanunua meza na viti 900 kugawa Shule za Sekondari
 
Huko Rukwa hakuna misitu?
halmashauri (Madiwani) wanashindwa nini kuidhinisha miti mitano ikatwe chap wanakijiji warande mbao wamalize tatizo au hata waombe wanakijiji wenye miti wajitolee miti....
Hii Nchi ina watu wanaotaka kila kitu wasaidiwe kufikiri na Rais au Waziri
 
This is Jamiiforums
Where we dare to talk openly
Asante kwa chapisho hili Mkuu, Wahusika wataliona na kutekeleza .
 
Huko Rukwa hakuna misitu?
halmashauri (Madiwani) wanashindwa nini kuidhinisha miti mitano ikatwe chap wanakijiji warande mbao wamalize tatizo au hata waombe wanakijiji wenye miti wajitolee miti....
Hii Nchi ina watu wanaotaka kila kitu wasaidiwe kufikiri na Rais au Waziri
Mkuu unaona wanakijiji wajitolee peke yao tu, We uoni kama pesa zetu zinatolewa kwenye Makanisa milioni mia mia bila sababu za Msingi huku Wananchi wanateseka, Wanatakiwa Viongozi wa Makanisa wao ndiyo watoe pesa kuchangia wananchi kwenye miradi ya kijamii ila wao wamegeuka ndiyo Wanapangiwa Bajeti ya Maendeleo na Ikulu na watoto wetu wana kaachini shuleni na Wagonjwa wa Figo Wasiokua na uwezo wa kusafisha Figo zao kuombo omba mitaani na uku Rais wao akigawa pesa kwa Maaskofu milioni Mia mia kwa kisingizio kuchangia ujenzi wa Kanisa wakati huo Watoto wetu wanakaa chini Mashuleni na wajawazito kulala kitanda kimoja hospitalini.
 
Maneno haya si mageni nchini labda Kwa mgeni malawi.
 
Achaneni na hayo mambo,tunzeni amani.

Chamsingi atafutwe afisa elimu wilaya unamtia bakora yeye na mkurugenzi wake
Mkuu wa wilaya na mkoa wanapigwa bakora
waziri anayehusika anapigwa mawe hadi afe
 
Mkuu unaona wanakijiji wajitolee peke yao tu, We uoni kama pesa zetu zinatolewa kwenye Makanisa milioni mia mia bila sababu za Msingi huku Wananchi wanateseka, Wanatakiwa Viongozi wa Makanisa wao ndiyo watoe pesa kuchangia wananchi kwenye miradi ya kijamii ila wao wamegeuka ndiyo Wanapangiwa Bajeti ya Maendeleo na Ikulu na watoto wetu wana kaachini shuleni na Wagonjwa wa Figo Wasiokua na uwezo wa kusafisha Figo zao kuombo omba mitaani na uku Rais wao akigawa pesa kwa Maaskofu milioni Mia mia kwa kisingizio kuchangia ujenzi wa Kanisa wakati huo Watoto wetu wanakaa chini Mashuleni na wajawazito kulala kitanda kimoja hospitalini.

Pamoja na kuwa na madini, mbuga za wanyama, bahari hadi leo kero katika huduma za jamii, maji, umeme, afya, elimu
 
Mwalimu kuwa makini. Serikali ya CCM haipendi kukosolewa hata kwenye mambo ya aibu kama haya.
 
Viongozi ndio wanastahili huduma bora. Wananchi wengine wajibu wenu ni kutunza amani.
 
Mkuu unaona wanakijiji wajitolee peke yao tu, We uoni kama pesa zetu zinatolewa kwenye Makanisa milioni mia mia bila sababu za Msingi huku Wananchi wanateseka, Wanatakiwa Viongozi wa Makanisa wao ndiyo watoe pesa kuchangia wananchi kwenye miradi ya kijamii ila wao wamegeuka ndiyo Wanapangiwa Bajeti ya Maendeleo na Ikulu na watoto wetu wana kaachini shuleni na Wagonjwa wa Figo Wasiokua na uwezo wa kusafisha Figo zao kuombo omba mitaani na uku Rais wao akigawa pesa kwa Maaskofu milioni Mia mia kwa kisingizio kuchangia ujenzi wa Kanisa wakati huo Watoto wetu wanakaa chini Mashuleni na wajawazito kulala kitanda kimoja hospitalini.

Kwa hiyo upo tayari mtoto wako akalie Ndoo darasani huku unasubiria Serikali?
Hilo lipo kwenye uwezo wa madiwani tu, kupitisha miti ikatwe na wanaweza kuuza hizo mbao kadhaa wakapata hela ya kutengeneza madawati na wala mwananchi hachangishwi..,...
 
Kwa hali hii basi hata vigogo wa serikali nao hawana sababu ya kupewa nyumba, magari, mafuta ya bure, nk. Si wajinunulie tu wenyewe! Mbona wana hela za kutosha?

Kwa nini tunachezea kodi za wananchi kiwahudumia? Mbona watumishi wengine wa serikali hawahudumiwi?
 
Watanganyika kodi zenu zinaijenga zanzibar. Nyie tunzeni aman sz. Kisha mkashabikie simba n Yanga.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Katavi ina mbao za kutosha Mkurugenzi na viongozi wengine hawafanyi kitu ili kutatua changamoto ndogo ndogo kama hizi..
 
Kwa hiyo upo tayari mtoto wako akalie Ndoo darasani huku unasubiria Serikali?
Hilo lipo kwenye uwezo wa madiwani tu, kupitisha miti ikatwe na wanaweza kuuza hizo mbao kadhaa wakapata hela ya kutengeneza madawati na wala mwananchi hachangishwi..,...
Madiwani hawamiliki Misitu na swala la kukata miti linahitaji maombi ya vibali kwenye idala usika, wewe kwa Utawala wa sasa kiongozi gani anaweza kukubali kusaini kibali kutoka Halmashauri cha kuomba kuvuna miti kwaajili ya Watoto?, Viongozi wa sasa wanafanya Majukumu yao yanayowaingizia pesa na hawafanyi Majukumu kwaajili ya Wananchi.
 
Licha ya jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia nchini, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipande iliyopo Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa Wanafunzi wanaendelea kusoma katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa madawati.

Shule hiyo ilianzishwa Mwaka 2006 na inatoa elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne. Hata hivyo, zaidi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, changamoto ya ukosefu wa madawati bado haijapatiwa ufumbuzi.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi hulazimika kukaa chini wakati wa vipindi darasani. Mazingira hayo si tu kwamba yanapunguza utulivu wa kujifunza, bali pia yanaweza kuathiri umakini, afya na matokeo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Wananchi na wadau wa elimu wanaeleza kuwa ni vigumu kufikia malengo ya kuboresha ubora wa elimu wakati wanafunzi wanalazimika kusomea sakafuni kwa kukosa samani za msingi kama madawati.

Wito kwa mamlaka husika, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kufanya tathmini ya haraka ya mahitaji ya shule hiyo na kuhakikisha inapata madawati ya kutosha ili wanafunzi wapate mazingira salama na yenye staha ya kujifunzia.

Elimu bora huanza na mazingira bora ya kujifunzia. Kukosekana kwa madawati katika shule iliyodumu kwa takribani miongo miwili ni changamoto inayostahili kushughulikiwa kwa haraka ili wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipande wapate haki yao ya msingi ya kusoma katika mazingira yanayowezesha kujifunza kwa ufanisi.
Mitano tena....Kazi na UTU...4Rs.
 
​

Mwalimu uwe makini sana nchi hii ngumu sana ccm hawataki kukoselewa utashangaa umetupiwa huko wampembe.
Ukiwauliza wanafunzi nani aliwapiga hiyo picha watakutaja
 
Back
Top Bottom