This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,198
- 5,454
Mheshimiwa waziri inaumiza kwa kitendo hiki cha Uongozi wa shule hii kuwakomoa vijana hawa wa kidato cha sita wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kitaifa mwezi May.
Kwa kifupi. Ni kwamba yalifanyika mahafali ya kidato cha sita juzi Jumamosi ya tarehe 5 Aprili 2025.
Mahafali yaliisha salama.
Ghafla jana Aprili 7, 2025 mzazi unapigiwa simu unaambiwa mwanao amesimamishwa masomo kwa siku 14. KOSA: ALILEGEZA SURUALI SIKU YA MAHAFALI.
Ikumbukwe mzazi ulikuwepo kwenye mahafali na hukuona hilo kosa.
MSINGI WA HOJA YANGU KAMA MZAZI NI HUU:
1. Waalimu wameishi na hawa vijana kwa miaka 2, sisi wazazi tumewatembelea mara nyingi, na hatukuwahi kuelezwa matatizo ya utovu wa nidhamu. Hana kumbukumbu zozote shuleni za utovu wa nidhamu. Isipokuwa siku ya mahafali.
2. Tufanye walitenda hilo kosa, Je, kwamba hilo ni kosa kiasi kwamba Uongozi wa shule ulikosa adhabu nyingine yoyote ya kuwapa? KWASABU KUMSUSPEND MWANAFUNZI WIKI MBILI MAANA YAKE NI MTOTO ALIYESHINDIKANA KWA UTOVU WA NIDHAMU.
3. Kuna wakati waalimu wanajisahau sana katika kufanya maamuzi. Wanawachukulia wanafunzi kama vile ni aina ya binadamu wasiohisi maumivu kabisa. Waalimu wanakuwa Wanyama na kuwafanya wanafunzi wao ni wanyama pia. Hata Simba pia ukimjeruhi huwa anafeel maumivu.
4. Halafu ni walimu hawa hawa vijana wakifeli unawakuta na wao wanasikitika wakati wao ni sehemu ya tatizo.
5. Naomba mheshimiwa Waziri kwanza tupewe ushahidi unaopita shaka kwamba hawa vijana walivaa hicho kinachoitwa Mlegezo. Tupewe ikibidi picha walizopgwa hawa vijana.
Ukiongea na baadhi ya walimu katika ile shule wengi wanasikitika kwa maamuzi ya uongozi wa shule ya kuwafukuza hawa vijana. Mmoja ameniambia shule ina bustani za kutosha za kulima ,ina shamba linahitaji palizi. Hizi ni adhabu zenye ufanisi ambazo wangeweza kupewa hawa vijana.
Badala yake kijana katoka Bukoba hana ndugu maeneo ya karibu kama Moshi, Arusha. Anapaswa arudi kwa wazazi wake Bukoba au Mbeya. Gharama ambazo hazikustahili kwa mzazi au mwanafunzi na hata ustawi wa shule pia.
Hii si sawa kabisa kuwakatili masomo vijana hawa 25 kwa maamuzi ya hovyo kama haya.
Nb: Hakuna mzazi anaependa kuona mtoto wake akiishi bila maadili. Lakini na hao wanaosimamia haya maadili kule shuleni basi wafanye maamuzi ya haki yanayozingatia weledi wa taaluma zao. WALIMU WAACHE KUKOMOA WANAFUNZI WAO. HILI NI TATIZO KUBWA SHULENI.
Je, Bodi ya shule nayo ilishiriki kufanya maamuzi haya?
Nauliza hili kwa sababu kwa uziefu wangu Mara nyingi haya yanafanywa na waalimu halafu Bodi inapewa tu taarifa baadaye.