Mheshimiwa waziri inaumiza na kwa kitendo cha Uongozi wa shule kuwakomoa vijana hawa wa kidato cha sita wanatarajia kuanza mitihani yao ya kitaifa mwrzi May.
Kwa kifupi.Ni kwamba yalifanyika mahafali ya kidato cha nne juzi Jumamosi ya tarehe 5 Aprili 2025.
Mahafali yaliisha salama.
Ghafla jana Aprili 7 mzazi unapigiwa simu unaambiwa mwanao amesimamishwa masomo kwa siku 14. KOSA: ALILEGEZA SURUALI SIKU YA MAHAFALI.
Ikumbukwe mzazi nilikuwepo kwenye mahafali na sikuona hilo kosa.
MSINGI WA HOJA YANGU KAMA MZAZI NI HUU:
1.Waalimu wameishi na hawa vijana kwa miaka 2,sisi wazazi timewatembelea mara nyingi hatukuwahi kuelezwa matatizo ya utovu wa nidhamu.Hana kumbukumbu zozote shuleni.
2.Tufanye walitenda hilo kosa, kwamba hilo ni kosa kiasi kwamba Uongozi wa shule ulikosa adhabu nyingine yoyote ya kuwapa? KWASABU KUMSUSPEND MWANAFUNZI WIKI MBILI MAANA YAKE NI MTOTO ALIYESHINDIKANA KWA UTOVU WA NIDHAMU.
3.Kuna wakati waalimu wanajisahau sana katika kufanya maamuzi. Wanawachukulia wanafunzi kama vile ni aina ya binadamu wasiohisi maumivu kabisa.
4.Halafu ni walimu hawa hawa vijana wakifeli unawakuta nao wanasikitika wakati wao ni sehemu ya tatizo.
5.Naomba mheshimiwa Waziri kwanza tupewe na ushahidi unaopita shaka kwamba hawa vijana walivaa hicho kinachoitwa Mlegezo. Tupewe ikibidi picha walizopgwa haw vijana.
Ukiongea na baadhi ya walimu katika ile shule wengi wanasikitika kwa maamuzi ya uongozi wa shule ya kuwafukuza hawa vijana. Mmoja ameniambia shule ina bustani za za kutosha za kulima ,liko shamba linahitaji palizi.Hizi ni adhabu zenye ufanisi ambazo wangeweza kupewa hawa vijana.
Badala yake kijana katoka Bukoba hana ndugu maeneo ya karibu kama Moshi, Arusha. Anapaswa arudi kwa wazazi wake Bukoba au Mbeya. Gharama ambazo hazikustahili kwa mzazi au mwanafunzi na hata ustawi wa shule pia.
Hii si sawa kabisa kuwakatili masomo vijana hawa 25 kwa maamuzi ya hovyo kama haya.
Nb: Hakuna mzazi anaependa kuona mtoto wake akiishi bila maadili.Lakini na hao wanaosimamia haya maadili kule shuleni basi wafanye maamuzi ya haki yanayozingatia weledi wa taaluma zao. WALIMU WAACHE KUKOMOA WANAFUNZI WAO.HILI NI TATIZO KUBWA SHULENI.