Sielewi kwa nini serikali za vijiji au kata hazina mipango madhubuti za kutatua tatizo kama hilo!! Nilitegemea wakati zinaanzishwa hizi shule, serikali za kata zingekuwa zimeshajipanga kuhakikisha zinatoa ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka maeneo yao kwenda hata private schools, au kwenda kufanya hata uchuuzi kwenye vyuo vya walimu kwa kuwavutia!!
Elimu ni kama uwekezaji siku hizi kutokana na tatizo kubwa la walimu, inabidi kuwavutia walimu!! hata hawa wanaohitaji fields au mazoezi basi kungekuwa na nyumba nzuri za wao kuweza kukaa bila malipo, wangekuwa wanapunguza tatizo.
Yote hayo yanahitaji viongozi wenye vision, wenye kujitolea siyo kuvizia watu wanaotaka kupiga watu faini ili wajenge nyumba zao.Wewe kwa vile umeweza kufika hapa jamvini, fanya kitu cha maana!! don't just sit there and do nothing, its for your ward, village and your neighbours!!
Itisha mkutano waeleze A - Z, nini kinatakiwa kufanya ili kuokoa watoto wenu katika kata ile.Naimani utafanikiwa na utakuwa shujaa wa hiyo kata, wilaya, mkoa pamoja na taifa. Kamwe usikatishwe tamaa na vikwazo utakavyokumbana navyo!! Undeni hata kamati ndogo huru ya watu wenye moyo safi kushughulikia hiyo inshu.
Unaweza hata kumwalika mkuu wa mkoa ukiona mambo yanaenda vizuri/vibaya hata waziri wa elimu. Kifupi mustakabli wa shule hiyo uko mikononi mwako kwani unaonekana una uchungu na hiyo shule. Kila la kheri.