Shule za A'Level Mpaka ngazi ya Kata/Tarafa

Shule za A'Level Mpaka ngazi ya Kata/Tarafa

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
1,130
Reaction score
2,102
Inasikitisha sana kuona serikali hii ya JK imeshindwa kabisa kuhakikisha walau kila wilaya hapa nchini inakuwa na shule ya A'level (Kidato cha tano & sita). Utashangaa Wilaya kongwe Mfano Halmashauri ya Morogoro pamoja na Ukerewe hazina Shule yenye A'level ya serikali. Halmashauri ya Morogoro ina A'level ya private moja tu (KIZUKA) wakati Ukerewe Hakuna hata moja. Hizo ni baadhi tu lakini wadau nadhani mtakuwa mnaelewa ninachomaanisha.

Katika dunia ya leo tunahitaji kuwa na shule za A'level mpaka ngazi ya kata ili angalau vijana wengi ambao kimsingi tumeadhimia elimu yao ya msingi ikomee kidato cha nne basi wapate nafasi ya kujiendeleza na kidato cha tano & Sita kupitia shule hizo.

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo hili linatakiwa kuwa miongoni mwa ilani za uchaguzi za vyama vya siasa ambavyo kimsingi viko mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo ya watanzania kwa ujumla.

Naomba kuwakilisha.
 
Mkuu hata hiyo serikali unayoifikilia kichwani ingekuwa madarakani bado kuna mapungufu ungeyaona tu, hakuna uongozi utakaoingia madarakani usije kutolewa kasoro, umetoa wazo zuri na hivyo kama walengwa limewafikia ni kulifanyia kazi tu. Binafsi nakuunga mguu sana ktk hilo shule za A'level ktk ngazi ya kata ni muhimu na zitasaidia wengi pia. Serikali izingatie hili mara moja plz.
 
Mkuu hata hiyo serikali unayoifikilia kichwani ingekuwa madarakani bado kuna mapungufu ungeyaona tu, hakuna uongozi utakaoingia madarakani usije kutolewa kasoro, umetoa wazo zuri na hivyo kama walengwa limewafikia ni kulifanyia kazi tu. Binafsi nakuunga mguu sana ktk hilo shule za A'level ktk ngazi ya kata ni muhimu na zitasaidia wengi pia. Serikali izingatie hili mara moja plz.

Kiuhalisia tuko nyuma ya muda. Ilitakiwa hili tuwe nalo tangu zamani lakini mpaka sasa baadhi ya wilaya bado ni ndoto. Tatizo kubwa ninaloliona ni siasa kuchanganywa na Elimu. Mfumo wa elimu yetu hauko huru na unabadilika kulingana na mahitaji ya wanasiasa. Rejea uanzishwaji wa shule za kata zilizopelekea upatikanaji wa walimu kwa njia ya Crash-Program maarufu kama vodafaster. Rejea pia shinikizo la ujenzi wa maabara kwenye shule za kata. Kwa hali hii system ya Elimu itaendelea kupelekwa pelekwa tu na wanasiasa kulingana na mahitaji ya kiongozi mkuu bila kuzingatia mahitaji ya Watanzania. Ni vema suala kama hili lingewekewa utaratibu mzuri wa kuliratibu na serikali ikaadhimia kama ilivyofanya kwenye sera mpya ya elimu. Lakini kwa sababu serikali inasukumwa na upepo wa uchaguzi mkuu, planning zote zinapotelea kusikojulikana ilimradi tu mgombea apate agenda mpya ya kumsindikiza. Tutasikia mara elimu bure, na si ajabu wanafunzi wakaahidiwa mpaka uji wa bure. Yote kwa yote ni ulaghai tu unaosumbua kizazi hiki.
 
Back
Top Bottom