SHULE ZA DAY(kata) ZA SERIKALI ZINAANGAMIZA TAIFA.

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,126
Ubovu wa matokeo ya kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na UWEPO WA SHULE ZA KATA,ambazo kimsingi zina mapungufu mengi sana ikiwemo walimu,vitabu na kukosekana kwa mabweni.

HIZI SHULE KUZIFANYA KUWA ZA DAY kumeongeza matatizo na ugumu kwa mwanafunzi kuliko zingekuwa za boarding(bweni)

ZINGEKUWA ZA BWENI kusingekuwa na tatizo la USAFRI. ZINGEKUWA ZA BWENI ingekuwa rahisi kutatua:-
1.tatizo la MAJI
2.tatizo la NISHATI ya kusomea(UMEME)
3.tatizo la MIMBA
4.tatizo la kuoa/kuolewa
5.tatizo la kukosekana kwa concetration kwenye kusoma na kujisomea.

INGEWEZEKANA KWA SABABU WANAFUNZI WAPO MAHALA PAMOJA.
 

Unataka kuniambia uwepo wa maji ktk sehemu fulani unategemeana na uwepo wa shule ya bweni ktk eneo hilo.?

Umeme nao hali kadhalika.?

Vipi uwepo wa walimu wa kutosha kwa shule hzo za day ambazo zngegeuzwa kuwa za bweni, wangejitosheleza?
 
Watoto wenyewe hawataki kusoma basi si lolote jengine hata waipewa nini hamna kitu.

Hapa inatakiwa shule zote ziwe chini ya jeshi wanafunzi wapige kwata amri tupu na bakora kwa anaefeli. Hata mwenyewe unaweza kujisomea kama unataka mwalimu darasani anakuonesha njia tu.

Tuziwekee hizi shule za serikali zote disciplinary offcers kutoka jeshini wanafunzi wapewe homework na asiefanya hakuna kurudi nyumbani mpaka umalize baada ya school hours, Lazima rushurutishe kusoma hakuna hiari tena taifa litaangmia kama hatutakua serious.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kutatua tatizo la maja kwenye shule yenye wanafunzi kwa mfano 400,haiwezi kuwa sawa na kutatua tatizo la maji kwa kila familia ya hao wanafunzi,wanafunzi wanapata shida ya maji na kutumia mda mwingi kutafta maji badala ya kusoma baadhi ya maeneo.

Vivyo hivyo umeme,umeme ni nishati ya kusomea na shule za kata zaidi 98% hazna umeme na maisha ya wanafunzi ni duni sana hvyo hawasomi usiku, matatizo ya usafri yanamalizwa na shule za bweni.

WALIMU HATA WALIOPO HAWAFUNDISHI,na kama ulibahatika kusoma shule za serikali iwe Olevel ama Advance huwezi kubisha hili,ila wanafunzi kwa mfano wa advance hawafeli kama fm4 kwa sababu advance zaidi 98% ya shule za serikali ni za bweni, WANAFUNZI WANAJISOMEA WENYEWE KIRAHISI KWA SABABU HAWANA MATATIZO YA USAFRI, UMEME, NA MAJI AMBAYO YANGEWAPOTEZEA MDA MWINGI NA KUKOSA UMEME, UKOSEFU WA VITABU NA VITABU VIBOVU NDIO SHIDA,ila walimu hata waliopo msaada wao ni sawa na hakuna mana ni wazembe kupindukia.
 

umeongea kinadharia zaidi..
1.tatzo la maji,ni bora kila m2 alitatue kwa jnc anavoweza yeye,hvo bora wakae day..kwan bwenn ndio litazd kuwasumbua zaid,hvo watazd kupoteza muda zaidi ktk kuyatafuta,kwa ajili ya kupikia nk.
2..hv hujui sababu inayowafanya advance kufanya vzr?hujui kuwa walichujwa wale thru necta fm4?
 
Mkuu umefanya utafiti au umesukumwa na fikra binafsi?
 
At GODIAN NGUNGUTI
Kwanza nikusahihishe kuwa KUNA VIWANGO VILIVYOWEKWA vya ufaulu ili mwanafunzi aweze kusoma advance.
VILEVILE kuna viwango vilivyowekwa ili mwanafunzi AWEZE KUJIUNGA FM ONE,
HIVYO UNAPOZUNGUMZIA MCHUJO WA FORM FOUR KWENDA ADVANCE UNAONGELEA WANAFUNZI WALIOTIMIZA VIGEZO KUJIUNGA NA FM 5.
hapo hapo unasahau kuwa hata kutoka shule ya msingi kwenda FORM ONE NAKO KUNA MCHUJO AMBAPO WALE TU WALIOTIMIZA MASHARITI KWA KUFIKISHA ALAMA ZINAZOHITAJIKA NDIO WANAENDA FORM ONE.
ama uliongelea mchujo gani ambao darasa la saba haufanywi kwenda fm one?
IKUMBUKWE KWA MFANO MWAKA JANA WANAFUNZI WALIOFAULU DARASA LA SABA WALIKUWA CHINI YA 60%,kati ya hao waliofaulu ndio walichagua baadhi kwenda fm one na wengine waliachwa,KATI 100% ya wanafunzi wote waliomaliza la saba ni chini ya 40% ndio walioenda form one.JE HAPA HAKUNA MCHUJO???

At MASAGWA
hoja yangu haihitaji kutumia nguvu nyingi mana mwenyewe nimepita huko.
ZAIDI KASOME FAIDA ZA KUWA NA SHULE ZA BWENI.na hata NYERERE hakujenga day ckul
 

unataka kuniambia kuwa hujawahi kusikia malalamiko kuwa watoto wanaenda
kdt 1 hata hawajui kusoma na kuandika?
unadhani advance ataenda mtu mwenye zero ili akawe kilaza kule?
vipi kuhusu kujitambua kwa mtu husika?unadhani tafsiri ya elimu
aliyokuwa nayo mtoto wa drs la 7 ni sawa na ile aliyekuwa nayo kijana wa
fm6?
kuhusu Jk wa kwanza kutojenga shule ya day ni kutokana na mfumo wa elimu uliokuwepo kwa kpnd kile ukilinganisha na idadi ya wasomaji..KWANI NI SHULE IPI YA BWENI JK 1 ALIIJENGA?
 
AT GODIANI.
Ninapozungumzia tatizo la maji kwanza ieleweke ni moja tu kati ya sababu zinazochangia wanafunzi kupoteza mda,WAKIWA BOARDING SERIKALI NDIYO INABEBA MZIGO WA KULETA MAJI KWENYE JUMUIYA YA SHULE NA KWA MAANA HIYO INAKUWA SI KAZI YA MWANAFUNZI TENA.
pia ikumbukwe tatizo hili linaathili zaidi wanafunzi wanaotokea vijijini ambapo hakuna vyanzo vya uhakika vya maji na wanasafri umbali mrefu zaidi ama wanalazimika kuamka usiku kufata maji.
KAMA UMEZALIWA NA KUKULIA MJINI UNAWEZA KUONA KAMA MZAHA.
najua kuna maeneo hawana tatizo hili ila sehemu kubwa ya nchi hili ni tatizo.
AMA NIAMBIE NI SHULE ZIPI ZA TOKA UTAWALA WA NYERERE ZA BOARDING HAZIKUWA/HAZINA HUDUMA YA MAJI NA UMEME AMA NISHATI YA UMEME WA UHAKIKA???

ukitaka kuhakikisha kuwa shule za kata za day ni janga FANYA MLINGANISHO WA MATOKEO YA SHULE za serikali MBILI ZIKIWA ENEO MOJA,shule moja ya day na nyingine ya boarding.
SIWEZI KUTOA MFANO BILA KUJUA UPO ENEO GANI,majibu utapata mwenyewe na kama yatapingama na maelezo yangu niwekee mfano huo
 

Kumbe wewe unazungumzia wakati wa utawala wa JK 1.?

UHALISIA.
Ktk utawala huu,jukumu la kutafuta maji ni la shule husika na wanafunzi wake..(nenda Namabengo sec schoo,namtumbo-ruvuma)utajionea ukweli ulivyo..
 
KUHUSU WATOTO WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA KWENDA FM1 NI KWELI NIMESIKIA SANA hata nimepata kusimuliwa na mwalimu mkuu mmoja.LAKINI TAMBUA HAPA NI UHALIFU UMEFANYIKA,ambapo bado uhalifu huu hauwezi kuwa umeathili matokeo kwa kiwango hiki cha dv zero 50%-2010, 47%-2011 na 60%-2012.
TAMBUA HATA kugushi vyeti olevel tatizo hili lipo na waliofeli wanaonekana walifaulu,na advance lipo pia ,,tena hapa napo nilipewa taarifa na lecturer m1 hapa nchini wakati walidahili mwanafunzi aliyekuwa na 4,lakini vyeti vyake ilikuwa dv2 na bila mwanafunzi mmoja kulalamika kwa nini yeye aliachwa akiwa na dv 3 ya 13 wakati mwenye 4 ya 18 kachaguliwa wasingejua na baada ya kufatilia walimtimua(MUHA.....)
moja ya shule zilizojengwa ktk utawala wa JK NI KIBITI,ipo pwani ila mifano zaidi mpaka nifatilie mana shule nyingi alitaifisha.
KUHUSU KUJITAMBUA.
tofauti ni kubwa advance wanajitambua kuliko primary na olevel.
LAKINI KUMBUKA KILA MWANAFUNZI KWA UMRI WAKE NA LEVEL YAKE ANATUNGIWA MTIHANI UNAOENDANA NAYE na hawafanyi mtihani SAWA
 
Kumbe wewe unazungumzia wakati wa utawala wa JK 1.?

UHALISIA.
Ktk utawala huu,jukumu la kutafuta maji ni la shule husika na wanafunzi wake..(nenda Namabengo sec schoo,namtumbo-ruvuma)utajionea ukweli ulivyo..

Kweli mkuu, sasa anataka waziri awapelekee maji kila shule!. Hivi wanajamii watoto wao wanao soma katika shule hizo wanafanya kazi gani?. Kwanini wasiboreshe mazingira wanayosomea watoto wao badala ya kuisubili serikali tu. Elimu ni gharama sana.
 
HIZO SHULE ULIZONITAJIA NI ZA BOARDING KAMA KIGONSERA AMA NI DAY?
hakika najua serikali hii imekwepa majukumu haya kwa sababu ya urahisi wa kuendesha shule za day NA NDIO MANA WALIONA WAZIFANYE SHULE KUWA ZA DAY.
NDIO MANA BADO NASEMA WAKIZIFANYA SHULE KUWA ZA BOARDING NA SERIKALI IKABEBA JUKUMU LA MAJI NA UMEME WATAKUWA WAMEWATATULIA WANAFUNZI MATATIZO NA USUMBUFU MWINGI.
 

mkuu,
ungejua madhara yanayotokana na watoto hawa wanaojiunga kdt 1 kisiasa,nadhani ungekubaliana na mimi,kiufupi,hawa ni tatzo,uelewa wao ni mdogo sana,nguvu nyng sana inahtajika japo kuwafanya waelewe kidogo,hvyo kufeli kwao wala sishangai...
 
At GODIANI GUNGUNGUTI.
kuhusu hoja yako ya uelewa mdo wa wanafunzi.
JE UNA MAJIBU YA MASWALI HAYA?
1.kwa nini ufaulu wa shule binafisi si mbovu kuliko shule za kata?
2.unajua kuwa shule za serikali ndizo huchagua wanafunzi waliofaulu vizuri zaidi iwe advance ama olevel na kuwaachia makapi shule binafisi?
3.kwa nini zamani wanafunzi walifaulu vizuri lakini sasa imeshindikana?
4.kwa nini shule za serikali za boarding zina matokeo mazuri kuliko shule za day za kata?
5.kama tatizo limesababishwa na mfumo mpya wa kuwapeleka watoto shule wakiwa na umri mdogo sana,KWA NINI
(i) shule za binafisi wanafanya vizuri katika umri ule ule?
(ii)kwa nini uganda watoto wa umri huuhuu wa primary walifaulu kwa 88% huku wa kwetu wakifaulu kwa 54% la saba mwaka jana?
Ama tanzania ni taifa la vilaza kwa sasa?
6.umewahi kufundisha hawa watoto unaowatuhumu ili kuthibitisha hoja yako?nimefundisha fm1 2012.WANAELEWA SANA ILA KAMA MWALIMU NI MZURI,Tatzo wameachwa kama watoto wa bata.
 

nitake radhi kwanza kwa kuniharibia jina langu hapo juu.
 
Shule za kata zina manufaa makubwa kuliko unavyo dhani.
Ni marekebisho kidogo ya ki mfumo/sera ya kufanyiwa kazi.
Watanzania wengi wamepata fursa ya kupata elimu kuliko ilivyokuwa mwanzo.
Hivyo hatua hiyo si ya kubezwa bali ni vizuri kuikosoa na kupata suluhisho sahii.
Mbatia ali puuzwa na Bunge,na hoja yake kutupwa kapuni,sasa unatarajia nini?
Kuna maoni na hoja mbalimbali ambayo wabunge wangeijadili bila kuzingatia itikadi zao
ambayo ingeweza kuinusuru Elimu yetu.Nikipata nafasi ningetoa mchango wangu wa jinsi ya kuiboresha.
 
Mimi nafikiri suala kubwa hapa ni maboresho ya shule hizi za kata kwasababu kuanzishwa kwake ilikuwa ni kwa madhumuni mazuri kabisa lakini kabla hazijakamilika mwasisi wake alijiuzulu ambaye alikuwa waziri mkuu bwana edward lowassa na sio hivyo tu bali zipo shule nyingine ambazo ni za kata na zina matokeo mazuri tu mfano shule ya sekondari mandaka iliyopo wilayani mwanga kilimanjaro ni shule mojawapo ambayo tangu imeanzishwa haina umeme maji ni shida majengo hayajakamilika lakini imekuwa ikifanya vizuri hivyo ni muhimu kuangalia umuhimu na maboresho yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…