Shule za English medium kufanya vizuri somo la kiswahili kwenye mitihani ya darasa la saba kuliko shule za swahili medium nini maana yake?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Ukiangalia matokeo ya darasa la saba 2019 kwa mfano shule za english medium ndizo zimeongoza kwa ufaulu kwenye somo la kiswahili kuliko shule zinazotumia lugha ya kiswahili kwenye masomo yote

Hii inamaananisha nini?

====


Pia raia wa China Congcong Wang aliongoza somo la Kiswahili ambalo alipata “B” Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2016, ambaye alishika nafasi ya pili kitaifa

Hali hii inaulizwa na wengi kushangaa hizi shule zinazotumia Kiswahili kufundishia masomo yote wanashindwa kufanya vizuri katika somo la Kiswahili.

Je kweli lugha ni kikwazo cha ufaulu, mbona watoto wa English medium hawaoni kiingereza kuwa kikwazo katika kufaulu Kiswahili
 
Hzo shule ziko vizuri kwenye nyanja zote...? Kwahyo fahamu hvyo..
 
Kiswahili cha kuongea sio sawa na cha mtihani. Vile vile kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia haikuhakikishii kufaulu SOMO LA LUGHA YA KISWAHILI.
 
Kiswahili cha kuongea sio sawa na cha mtihani. Vile vile kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia haikuhakikishii kufaulu SOMO LA LUGHA YA KISWAHILI.
Sasa kinacho badilika sana katika hapo..... hizo lame excuse kama za waziri Dalichako eti ana PhD ya mathematics eti ndomaana anakisea kuongea kiingereza vizuri........kule st kayumba 80% hamna ufundishaji ni sehemu ya kusukuma miaka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sielewi unaongea nini kulingana na nilichoandika. Mara Ndalichako, mara excuse.
 
Watoto wanaosoma English Medium wanauwezo mkubwa wa kukariri kiswahili kuliko hawa wanaosoma Kanumba PSs
 

Kwanza hawafundishwi hicho Kiswahili kwa kiingereza lakini pia wamefanyaje kwenye masomo mengine ambayo hufundishwa kwa Kiingereza?

Walimu tunaujua ugumu wa kumfundisha mtoto ambaye lugha yake ya kwanza ni Kiswahili kwa Kiingereza lazima ugeuke mfasiri wa somo ndipo ueleweke.
 

Unazungumza kama mtaalamu au kama mtu wa kawaida? Unafahamu tafiti zimefanyika na kuthibitisha kuwa matumizi ya lugha ya Kiingereza kufundishia kunakwamisha sana wanafunzi kupokea maarifa?

Unavyoona wewe ili kupata jeuri ya kukutumia Kiswahili kufundishia tunahitaji nini ambacho hatuna?
 
Ukiangalia wanafunzi wengi haswa wa shule za Kata, wanajifunza kiswahili na Kiingereza kwa kutamka maneno ya mkato au ya kufupisha bila na wanaenda kuyatumia katika mitihani, mtu akisikiliza muziki wa Bongo Flavour namna wanvyoharibu lugha na watoto wananakili na kuweka vichwani mwao
 
Moderators wanahariri comments mpaka zinakosa ladha!

Hakuna uhuru wa kujieleza! Kila ukiandika wanahariri wanajaza ya kwao!!

Kichefuchefu tupu!

Basi tuwaachie jukwaa lenu mjaze contents mnazozitaka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…