Shule za English Medium za Serikali: Mwanya Mwingine wa Upigaji Pesa za umma

one one chief

Member
Joined
Jan 22, 2014
Posts
39
Reaction score
105
Katika miaka ya karibuni, halmashauri nyingi nchini Tanzania zimeanza kuanzisha shule za serikali zinazotumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia kuanzia darasa la kwanza maarufu kama “English Medium Schools.” Lengo likiwa kuongeza ubora wa elimu, kutoa ushindani kwa shule binafsi, lakini pia kutoa fursa kwa watoto wa familia za kipato cha chini kupata elimu bora.

Hata hivyo, hali halisi inavyoonekana sasa inatoa taswira tofauti, huku baadhi ya shule hizi zikitajwa kuwa vyanzo vya mapato yasiyo na udhibiti wa kutosha na hata kuwa mianya ya upigaji wa fedha za umma.

Ni kweli kwamba ubora wa mazingira ya shule, nidhamu ya walimu, na lugha ya Kiingereza kama njia ya kufundishia huwavutia wazazi wengi. Lakini shule hizi zimekuwa kibiashara zaidi kuliko kijamii. Shule hizi zimekuwa Zikitangaza udahili wa wanafunzi kwa madarasa ya awali na msingi kisha hufuatiwa na usaili ambapo wazazi hutozwa ada ya usaili bila risiti halali, na mara nyingine hata nafasi huuzwa kwa ‘wanaojulikana.’

Fedha zinazokusanywa kupitia ada, michango ya sare, chakula, na maendeleo mara nyingi hukusanywa moja kwa moja na uongozi wa shule. fedha hizi hazipelekwi kwenye akaunti kuu za serikali au hazijumuishwi kwenye bajeti ya halmashauri, jambo linaloleta mashaka kuhusu uwazi wa matumizi.

Shule za English Medium za serikali ziliundwa kwa dhamira njema ya kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu. Hata hivyo, bila mfumo wa udhibiti wa ada, uendeshaji, na usimamizi wa fedha zinageuka kuwa mianya ya kujipatia fedha kwa baadhi ya watendaji.

Serikali kuu inapaswa kuingilia kati kwa kuweka miongozo thabiti, ukaguzi wa mara kwa mara, na ushirikishwaji wa jamii ili kuhakikisha shule hizi zinarudi kwenye misingi ya kutoa elimu bora kwa wote.
 
Kama huna hela ya kumpeleka mwanao shule private achana na hizi wanazosema English medium za gavoo wewe mpeleke tu shule uliyokarabu nayo.
 
Umeelewa kweli alichoandika?
Nimeelewa mkuu ( yeye alikuwa anazungumza kuhusu mismanagement ya pesa na ukusanyanyi wa pesa usioleweka kwenye hizo shule) hii nimetoa tu ushauri Kwa wengine, maana mkuu maana elimu inayotolewa kwenye hizo shule bado duni
 
Sawa. Hoja yake ni mismanagement ya public funds ambapo haijalishi ana mwanafunzi au hana
 
Back
Top Bottom