A
Anonymous
Guest
Shule za msingi Njombe Mjini (sio zote) zimekuwa zikitoza hela ya mitihani kwa wanafunzi wake elfu 5 hadi elfu 10 kwa mtihani mmoja kila wiki na kwa wale wanaochelewa kulipa walimu na wakuu wao husema hela inahitajika maana hata wao wanadaiwa na halmashauri hela za mitihani ndio maana na wao wanadai kwa wazazi.
Ukiangalia mitihani yenyewe wanayosema wanauziwa na halmashauri ni ile ambayo imefanywa na halmashauri nyingine hapa nchini na unaweza ukaichukua kwenye internet na ukizingatia shule ina photocopy machine ila bado wanatoza kiasi kikubwa cha pesa kwa wazazi ukizingatia hata ukitoa hiyo pesa hupewi risiti na hujazwi kwenye daftari badae unaambiwa hujalipa.
Je, Halmashauri ya Njombe mjini yenyewe inahusika moja kwa moja kwa hili linaloendelea kwenye shule zake za msingi? Na kama inahusika haiona kama inawakandamiza wazazi kwa kiasi kikubwa cha pesa kwa mtihani ambao sisi wazazi tunai-download Telegram?