A
Anonymous
Guest
Mimi ni mzazi ninayesomesha watoto zaidi ya wawili katika shule za sekondari za umma katika halmashauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kero yangu kubwa ni kukithiri kwa michango mbalimbali kwenye hizi shule japokua baadhi ina tija ila hofu yangu ni uwezo wa wazazi kuimudu.
Wanafunzi wengi wa hizi shule wanatokea familia za hali ya kati au chini kabisa (maskini) na lengo la serikali kufuta ada na michango ni kuwawezesha wanafunzi wote kupata fursa ya masomo bila kujali hali zao za kiuchumi.
Ila kwa michango tunayolipa kwa sasa ni bora serikali irudishe tu ada ya kiasi cha 40000/= au 20000/= kama zamani maana kwa mfano mwanangu anaesoma shule ya Nyamanoro sekondari anatakiwa kulipa kila mwezi 6000/= kwa ajili ya masomo ya ziada (remedial) ambapo kwa mwaka mzima hapo analipia miez 9 ya masomo ambayo ni kiasi cha shilingi 54000/= kisha anatakiwa kuchangia hela ya chakula 1000/= kwa siku, hapo bado mzazi hajatoa nauli ya mwanafunzi kwenda shuleni na kurudi nyumban.
Ukijumlisha kwa mwaka hicho ni kiasi kikubwa cha pesa na inaondoa maana halisi ya elimu bila malipo.ukienda shule ya kiloleli napo michango ipo kama yote.
Wito wangu ni kuiomba serikali isimamie hii michango maana imekua mingi sana na kama itaonekana ni busara bora turudi kulipa ada kama zamani na kupunguza michango hii ya mara kwa mara.