Mkuu, hili suala la vipaji maalumu hata mimi nashindwa kuelewa mantiki yake ni nini hasa. Hii ni ishara ya kufeli kwa serikali katika kushughulikia matatizo ya elimu yanayoisibu nchi yetu. Niliwahi kuandika mada hii kupitia magazeti ya Nipashe na Mwananchi kama ifuatavyo na watu wengi waliniunga mkono katika utetezi wangu huu. Lakini mada hiyo nilipoiweka humu JF sikupata uungwaji mkono wa kutosha na watu wengi waliniponda kwa kutoona umuhimu wa shule za 'vipaji maalum'. Inashangaza kwamba kufaulu vizuri mitihani (hata kama umeiba mitihani), kwa Tanzania hiki ni 'kipaji maalum'!