Shule zote, Vyuo vikuu na Nyumba za Ibada, zipewe Ulinzi wa kutosha

Shule zote, Vyuo vikuu na Nyumba za Ibada, zipewe Ulinzi wa kutosha

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
Imefikia mahala lazima serikali ijihami ipasavyo kulinda raia zake baada ya magaidi wa Al shaabab kuweka kambi nchi ya jirani msumbiji.

Uharibifu wa mali ya uma,, wingi wa vifo na kutimuliwa katika makazi yao raia wa msumbiji si kitu cha kusikiliza kama mechi ya soka bila kukifanyia kazi na kujihami kwa mbinu azizi.

Inasikitisha sana leo hii wakazi wengi sana wa Msumbiji wanaishi katika matenti kama skauti bila hiari yao baada ya hawa magaidi kuwatia hasara ya uhai na mali zao.

Nimetaja sehemu nyeti sana ambazo mara kwa mara magaidi hutumia kama soft target ili kuimiza serikali na kutuletea uchungu raia wa wapenda amani.

Serikali za kiafrika hazijishughulishi kumtafuta nani nawafadhili hawa magaidi kwa kuwapa pesa na siraha na magari bali nchi zetu zinapeleka majeshi ya kulinda amani tuu.

Sasa watapeleka majeshi ya kulinda amani mpaka lini ikiwa kama kuna watu matajiri wanawachangia hela magaidi au nchi fulani zinawapa misaada kisirisiri .

Mungu ibariki Tanzania!
 
Ni jambo Muhimu sana kama tukijihami kuliko hasara itakayokea bila kutarajia maana maumivu ya kichwa huanza taratibu na usipotibu mwishowe kifo!
 
Hivi ni kwa nini wanaua raia wa kawaida?

Lengo lao ni nini?Na anayewapa misaada kufanya haya anafaidika na nini?
 
Imefikia mahala lazima serikali ijihami ipasavyo kulinda raia zake baada ya magaidi wa Al shaabab kuweka kambi nchi ya jirani msumbiji.Uhalibifu wa mali ya uma,, wingi wa vifo na kutimuliwa katika makazi yao raia wa msumbiji si kitu cha kusikiliza kama mechi ya soka bila kukifanyia kazi na kujihami kwa mbinu azizi. inasikitisha sana leo hii wakazi wengi sana wa msumbiji wanaishi katika matenti kama skauti bila hiari yao baada ya hawa magaidi kuwatia hasara ya uhai na mali zao.

Nimetaja sehemu nyeti sana ambazo mara kwa mara magaidi hutumia kama soft target ili kuimiza serikali na kutuletea uchungu raia wa wapenda amani. serikali za kiafrica hazijishughulishi kumtafuta nani nawafadhili hawa magaidi kwa kuwapa pesa na siraha na magari bali nchi zetu zinapeleka majeshi ya kulinda amani tuu. sasa watapeleka majeshi ya kulinda amani mpaka lini ikiwa kama kuna watu matajiri wanawachangia hela magaidi au nchi fulani zinawapa misaada kisirisiri .

Mungu ibariki Tanzania!
Bila kusahau bwana yule kapeleka majeshi yake haraka haraka huko bila ruhusa ya SADC kila nchi inamshangaa vipi anamission gani hapo inayomfanya awahi bila wenyeji wake..nchi tuwe makini Sana Sina Imani na Rwanda kabisa..
 
Hivi ni kwa nini wanaua raia wa kawaida?

Lengo lao ni nini?Na anayewapa misaada kufanya haya anafaidika na nini?
Sioni tofauti ya WACHAWI na hivi vikundi vya kigaidi, sema wanatofautiana vitendea kazi tu, wachawi wanatumia matunguli wakati magaidi wanatumia vifaa vya kisasa but wote wana KIU ya damu za binadamu
 
Back
Top Bottom