Shutuma dhidi ya ndugai zilitakiwa kuibuliwa na bunge, na msamaha ulitakiwa kuombwa kwa bunge na wananchi.

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Kongole wanaJF.......kutokana na spika kuwajibika kwa bunge na wananchi, ikiwa matamshi yake yalikiuka mwenendo, sheria na taratibu za bunge, shutuma hizo zilitakiwa kuibuliwa na bunge lenyewe na kama ni kuomba msamaha ndugai alitakiwa aombe huo msamaha kwa bunge au moja kwa moja kwa wananchi. Hili lililotokea kwa mhimili mmoja kuomba msamaha kwa mhimili mwingine kunaleta dhana potofu ya uhuru wa kimamlaka ya hii mihimili.
Nawasilisha.​
 
Mamlaka ni moja tu na ndio uhalisia wake nao ni uliojichimbia
Mengine ni Screen tu Remote ipo na wenye akili wanalijua hili full stop,
 
.... sawa but is that the standard operating procedure as per the Constitution?
 
Kongole wanaJF.......kutokana na spika kuwajibika kwa bunge na wananchi, ikiwa matamshi yake yalikiuka mwenendo, sheria na taratibu za bunge, shutuma hizo zilitakiwa kuibuliwa na bunge lenyewe na kama ni kuomba msamaha ndugai alitakiwa aombe huo msamaha kwa bunge au moja kwa moja kwa wananchi. Hili lililotokea kwa mhimili mmoja kuomba msamaha kwa mhimili mwingine kunaleta dhana potofu ya uhuru wa kimamlaka ya hii mihimili.
Nawasilisha.​

Shutuma alipeleka kwa Rais. Alianza na Neno "mama juzi hapa ameenda kukopa" Ina maana alimlenga Rais.
 
Sasa kama swala la kumsema rais lilikiuka taratibu, kanuni au sheria za bunge analoongoza, bunge lenyewe ndo lilitakiwa kuja na shutuma dhidi yake, sijui kama umenielewa.....
 
Back
Top Bottom