SHUTUMA: Jay Msangi awawekea madawa mabondia wa Tanzania ili wapoteze pambano

SHUTUMA: Jay Msangi awawekea madawa mabondia wa Tanzania ili wapoteze pambano

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Promota mkubwa wa ngumi hapa nchini Tanzania ,JAY MSANGI anashutumiwa kuwawekea madawa mabondia Ibrahimu Classic pamoja na mwenzake Adam Mbega.

Shutuma hizo zilitolewa na bondia Ibrahimu Classic kwa kudai kuwa Jay alihusika moja kwa moja kumuwekea yeye madawa ili asiweze kuona vizuri dhidi ya mpinzani wake ambaye walikuwa wanawania mkanda wa WBO, pia Ibrahimu alidai kuwa JAY alihusika pia katika kumuwekea madawa Adam Mbega ili ashindwe kufanya vizuri katika pambano lake ambapo alimsababishia matatizo ya tumbo Adam.

Mbali na hao Jay Msangi pia anahusishwa katika kumuhujumu bondia mwingine aitwae Muhsin Kizota kwa kufanya figisu figisu ili tu Muhsin apoteze pambano .

Mpaka mwisho wa pambano Ibrahimh Class alipoteza pambano round ya saba kwa Technical Knockout, Muhsin Kizota alipoteza pambano kwa Technical Knockout round ya sita na Adam Mbega alipoteza pambano kwa points round nane.


Mbaya zaidi JAY MSANGI aliamua kukimbia na pesa za mabondia hao.

Mbali na mabondia hao, mabondia wengi wamekuwa wakimshutumu Jay Msangi mara kwa mara kwamba yeye ndiye kisababishi kikuu cha wao kupoteza mapambano .

Inavyosemekana Jay Msangi huwalazimisha mabondia wakubali kupigwa na wazungu ili waongezewe dau na kama itatokea bondia akikataa kupigwa Jay atafanya kila ajualo yeye ili tu wabongo wapoteze pambano na hivyo kuwatengenezea wazungu rekodi nzuri za mapambano yao.


*********************************************


Ila kiukweli hata mimi huyu Jay Msangi nilikuwa nina mashaka naye sana kwa kipindi kirefu ,kwa sababu haiwezekani kila akiondoka na bondia hapa nchini huyo bondia lazima apoteze iwe isiwe,sijawahi kusikia au kuona hata mara moja Jay akisafiri na bondia halafu huyo bondia akashinda hilo pambano.


Mamlaka husika embu ingilieni kati hili suala .


20181211_194352.jpeg
20181211_194413.jpeg
20181211_194331.jpeg
 
Huyu Msangi kwenye shutuma hua haziishi kabisa, lakini ni yeye ambaye hutafuta mapambano kwa hao bondia,
Ila Mabondia wetu wanahitaji shule kidogo, kama huyo Classic[emoji849]
 
Huyu Msangi kwenye shutuma hua haziishi kabisa, lakini ni yeye ambaye hutafuta mapambano kwa hao bondia,
Ila Mabondia wetu wanahitaji shule kidogo, kama huyo Classic[emoji849]
Shule na ngumi wapi na wapi????


Floyd Mayweather hajasoma lakini huwezi kutaja mabondia wenye mafanikio ya ulingoni na mafanikio ya kimaisha halafu usimtaje Floyd Mayweather.
 
Tafuteni wanasheria/manager wa kuwasimamia kazi kazi,bondia hata kuandika kiswahili inakuwa shida lazima utaibiwa
 
Huyu Msangi kwenye shutuma hua haziishi kabisa, lakini ni yeye ambaye hutafuta mapambano kwa hao bondia,
Ila Mabondia wetu wanahitaji shule kidogo, kama huyo Classic[emoji849]
Mayweather hajui kusoma wala kuandika hata Mike Tyson.Classic mbona kajitahidi kwa shule za kata..
 
Mayweather hajui kusoma wala kuandika hata Mike Tyson.Classic mbona kajitahidi kwa shule za kata..

kweli, lakini Mayweather na Tyson hawawezi kusema "nimewekewa madawa machoni na promoter wangu nikapata upofu na tumbo la kuharisha..."

watamuuliza promoter ndio mpishi wako?

and what was the motive, ushindwe ili iweje? Oooh, ili tushindwe ili wazungu wapate rekodi nzuri, mzungu akipata rekodi Juma anafaidika vipi, Juma Msangi mzungu?

kwa hiyo huwezi kulinganisha shule ya mtaani ya Mayweather na Tyson na hawa wa kwetu hawa, mtu ambae hajaenda shule Marekani ukikatana nae barabarani anakuwa na upeo wa uchambuzi wa mambo kama au kuzidi PhD wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom