Shutuma mpya kwa CHADEMA, wanachama wa Zanzibar wanadai Ruzuku pamoja na kupinga ubaguzi wa Dini, Ukabila & Muungano

Shutuma mpya kwa CHADEMA, wanachama wa Zanzibar wanadai Ruzuku pamoja na kupinga ubaguzi wa Dini, Ukabila & Muungano

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,651
Reaction score
1,129
Shutuma mpya kutoka kwa CHADEMA Zanzibar wanadia kuwa CHADEMA haipeleki Ruzuku Zanzibar

Wanachama wa Zanzibar hawaishii hapo vilevile wanadai kuwa CHADEMA imekithiri ubaguzi wa dini wakidai kuwa tangu kuanzishwa kwake haijawahi kumpa nafasi ya uenyekiti mwanachama wake wa dini ya Kiislamu

Wanadai kuwa pamoja na yote hayo kuna tatizo la ukabila, viongozi wake wakubwa wanatokea Kaskazini na kati mwa Tanzania

Kubwa zaidi wanadai CHADEMA haipendi kujihusisha na Zanzibar mara zote imekuwa ikizungumza habari za Tanganyika kana kwamba hakuna Muungano
 
Wanataka ruzuku sawa wao wanachangia nini.
Toka chama kianzishwe wamewahi kutoa mbunge ukiachiliwa wa kuteuliwa.
Mwenyekiti anachaguliwa kwa kupigiwa kura au dini yake.
 
Wanataka ruzuku sawa wao wanachangia nini.
Toka chama kianzishwe wamewahi kutoa mbunge ukiachiliwa wa kuteuliwa.
Mwenyekiti anachaguliwa kwa kupigiwa kura au dini yake.
Wanataka pasu kwa pasu 😁
 
Wako sahihi kabisa. CHADEMA kinajitambulisha kama chama cha kikristo hivyo kuwabagua waziwazi waislamu. Mara nyingi hiki chama kimejiegemeza kwa wachungaji na mapadri hivyo kukipa taswira ya kuwa dini ya kikristo. Kwa chama kinachotaka kushika dola kwenye nchi yenye waislamu zaidi ya 30% ya population kinakosea sana kuwabagua waislamu. Bagonza, Mwamakula na Kitima wana mchango mkubwa kukikosesha CHADEMA uungwaji mkono na waislamu.
 
Back
Top Bottom