Elections 2010 Shy-Rose Bhanji amvaa Idd Azzan

Elections 2010 Shy-Rose Bhanji amvaa Idd Azzan

Mdondoaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Posts
5,108
Reaction score
1,137
MENEJA Uhusiano wa Benki ya NMB, Shyrose Sadruddin Bhanji, amejitosa kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuwa kiungo katika jamii ya wana Kinondoni.

Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Bhanji alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kwani kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo.

Bhanji alibainisha mambo makubwa ambayo atayapigania kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ni elimu, afya, ajira kwa vijana, kupiga vita utumiaji wa dawa za kulevya kwa vijana, kupigania haki za wasanii, kusaidia wajane katika kujikwamua kiuchumi na kuleta msukumo mpya kabisa katika masuala ya mahusiano na jamii ambayo kwa mtazamo wake eneo hili linahitaji msukumo.

Alisema sababu ingine iliyompa ujasiri wa kujitokeza katika nafasi hiyo ni kutokana na kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi akiwemo Rais Jakaya Kikwete, za kuwataka wanawake kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ili Tanzania iweze kufikia hatua ya kuwa na wabunge asilimia 50 wakiwa ni wanawake.

Shy-Rose amepata kuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya serikali ya Daily News, mtangazaji Televisheni ya Taifa (sasa TBC1), Meneja Uhusiano Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB, nafasi anayoshikilia hadi sasa tangu mwaka 2006.

“Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananchi” alisema.

Source: Tanzania Daima

Mwaka huu kazi ipo haki ya Mungu kila mtu mwanasiasa!!!!
 
This time dada atashinda in case hakuna mwanaCCM mwingine atajitokeza... maana Iddi Azzan ni kimeo.
 
Hata mimi nitamuunga mkono kwani anaweza kuleta mabadiliko kwenye eneo la Kinondoni kwa jinsi ninavyomfahamu Shy-Rose Bhanj, maana Kinondoni kuna uozo unaohitaji juhudi binafsi
 
Ah,she made a wrong choice.Majimbo ya Dar ni magumu sana.However,akipata sapoti ya mwenye nchi (JK) anaweza kushinda.
 
Hata mimi nitamuunga mkono kwani anaweza kuleta mabadiliko kwenye eneo la Kinondoni kwa jinsi ninavyomfahamu Shy-Rose Bhanj, maana Kinondoni kuna uozo unaohitaji juhudi binafsi

Watanzania wenzangu, kwa nini hatutaki kuelewa MAENDELEO YA WATANZANIA YATALETWA NA WATANZANIA.

Maendeleo ya Kinondoni yataletwa na Wana Kinondoni, sio Mbunge.
 
Ah,she made a wrong choice.Majimbo ya Dar ni magumu sana.However,akipata sapoti ya mwenye nchi (JK) anaweza kushinda.

Kwanini hakuenda vijijini ambapo rahisi kushinda?
 
Ah,she made a wrong choice.Majimbo ya Dar ni magumu sana.However,akipata sapoti ya mwenye nchi (JK) anaweza kushinda.

Kwanini hakuenda vijijini ambapo rahisi kushinda?

Mlalahoi na Mdondoaji,

Nashindwa kuelewa fikra zenu zinafikiria nini. Mgombea anaishi Kinondoni, ila nyie mnapendekeza akagombea Mkoani kwa sababu ni rahisi kushinda, mnacho onekana mnapendekeza hapa ni kuwa Bora Kushinda Ubunge na wala sio uwepo wako Jimboni ili kuwaelewa na kuwatumikia Wapiga kura wako.!!

Kweli tuko serious kwenye kutaka nchi yetu ibadilike?
 
Watanzania wenzangu, kwa nini hatutaki kuelewa MAENDELEO YA WATANZANIA YATALETWA NA WATANZANIA.

Maendeleo ya Kinondoni yataletwa na Wana Kinondoni, sio Mbunge.

Kulikuwa hakuna sababu ya kuwepo na chaguzi za madiwani, wabunge, hata Marais kwani kama marais wananchi husika wangeleza maendeleo!! Hata kwenu bila baba yako hakuna maendeleo labda uwe umeshaanza kujitegemea lakini kama utakuwa kwa baba ni baba pekee wa kukuletea maendeleo!!

Wabune ni wa wakilishi wetu katika serikali kwakuwa hatuwezi kila mmoja pale Magogoni kueleza shida zetu, lazima tuwe na mtu wakutuwakilisha katika chombo kinachotoa maamuzi!!

Kama ni wa Kinondoni ungekuwa unajua kwanini meneo mengi ya wazi yameuzwa na mpo mnaona mpaka alipokuja mkuu wa mkoa tena katokea Dodomaaa!! Na kuanza kufanyia kazi kero mbalimbali ikiwemo uuzaji wa maeneo ya wazi.
 
Ah,she made a wrong choice.Majimbo ya Dar ni magumu sana.However,akipata sapoti ya mwenye nchi (JK) anaweza kushinda.
😛ound:😛ound:😛ound:atashinda tu, wether you like it or not!
 
😛ound:😛ound:😛ound:atashinda tu, wether you like it or not!

Akipita tu katika kura za maoni tu!! let her try her opportunity! ni haki yke kikatiba!
:lol:
 
Ama kweli dunia kubwa..Shay Rose mdogo wangu leo hii agombea ubunge Kinondoni atamweza kweli JP (Jumaa) nasikia naye kachukua form.
 
Ah,she made a wrong choice.Majimbo ya Dar ni magumu sana.However,akipata sapoti ya mwenye nchi (JK) anaweza kushinda.

Hakuna jimbo rahisi kuchukua Dar kama Kinondoni... kama Iddi Azzan alishinde then anybody can.
 
Ah,she made a wrong choice.Majimbo ya Dar ni magumu sana.However,akipata sapoti ya mwenye nchi (JK) anaweza kushinda.

Mkuu magumu kama ukigombea kwa tiketi upinzani, maana wenye nchi wana sera yao kuwa kitovu kikuu cha uchumi nchini hakiwezi kuwa chini ya upinzani. 1995 majimbo yote yalishikwa na upinzani wakavuruga uchaguzi na kurudiwa baade baada ya kupa formula ya ushindi. Yaani jitatangaze umeshimda hata kama kura hazipo!
 
Wabongo bana na upuuzi wao wa siasa uchwara, ni kama mgonjwa na uji.
 
People have been going bananas over these siasa uchwara na usanii!
 
- Hivi SHY-ROSE ni "AFUKASTI"?

- She may be part of a "STRATEGIC PLAN" led by Sir C!
 
IDD AZZAN lazima aingie mitini hakusoma amegushi cheti cha form 4 kupata ubunge.Ingawa ni kawaida ya wana CCM kughushi kila kitu.
 
Back
Top Bottom