07/08/2010
Picha na maelezo kwa hisani ya Wavuti.com
Takriban miaka Hamsini tangu tujiite kuwa Huru (nusu karine inaingia) Angalia hiyo picha naamini itakukumbusha nyingi ulizoziona hapa na kwengineko. Zifikirie Huduma za Afya, Elimu, Usafiri nk.
Mfikirie Raisi wako na Mawaziri wake, wafikirie Wabunge wetu na Maafisa wakuu wa serekali, mkumbuke Benjamin Mkapa, Chenge, Lowasa, Ndilu na wale wa aina yao, halafu ingalie tena hii Picha. Najua hatuko sawa na wala hatuwezi kuwa sawa, lakini ni wazi kuna Mstari unakosekana mahali, mstari wa Uwiano umekiukwa vibaya, tena vibaya sana, kwa Waumini wa Dini wanaweza kudai kuwa tumo katika Kukufuru, na ndio maana nauliza MAPAMBANO YANAANZAAAA? AU YANAENDELEAAAAA!!!!!! 50 YEARS ON....
Shy-Rose Bhanji, Handeni, Tanga
Ni jambo la heri kutembelea watu katika maeneo ya vijijini ili kupata uhalisia wa maisha huko kwa ajili ya kujipanga vyema na kuwa sauti yao katika kufikisha mahitaji yao katika ngazi husika za uongozi, pia kupanga na kuandaa mikakati ya kuwakwamua katika mazingira magumu ili nao wajisikie kuwa sehemu ya jamii inayofurahia huduma muhimu kama vile maji, umeme, barabara, shule nk.
Hongera Shy-Rose.