Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 233
Jamaa sielewi miaka mitano bungeni amefanya nini?Kuhusu Kidato cha nne amefika,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.IDD AZZAN lazima aingie mitini hakusoma amegushi cheti cha form 4 kupata ubunge.Ingawa ni kawaida ya wana CCM kughushi kila kitu.
Jamaa sielewi miaka mitano bungeni amefanya nini?Kuhusu Kidato cha nne amefika,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Hebu angalia hii ni moja ya shule za msingi hapa Tz huko mkoani Shy, nahii ni baada ya miaka 49 ya uhuru.
kwa mujibu wa duru za siasa za ccm - kinondoni, ukweli ni kwamba jamaa ana wakati mgumu sana, ufanisi wake ni hafifu mno ... anapata wakati mgumu sana kujibu maswali ya maendeleo kwenye vikao vya ndani vya chama ... na inasemekana hata mkulu amehoji hilo na wenyewe wanadai atashangaa sana kama jamaa atapitishwa na wanachama wa kinondoni! Miezi michache alianza kujenga mtandao wa vijana na kuwakatia mshiko ili waweze kumjengea ushawishi wa kurudi "mjengoni" lkn nasikia ame-back off baada ya mbinu zake kushtukiwa kwani amekuwa akifanya hivyo bila ridhaa ya chama - kindondoni!
Kuhusu Shy-rose nasikia hana ushawishi sana lkn kwa sasa ndio hivyo tena ni bora liende sababu mbunge mwenyewe ndio hivyo ... inasemekana pia huyu dada anatumia msuba (ganja) ... dah hawa wabunge wetu??!! na asipotoka mshindani wa ukweli huyu dada anaweza shinda kura za maoni sababu ni wazi kwa sasa Idd Azan hauziki kabisa na huyu dada anaweza onekana ana afadhali ... otherwise sijui iweje!
Bottom line ni kwamba jimbo la kinondoni might again become a loosing side for the next "whooping" five years!
at least wana madawatiDom,
Shy, Inasimama kwa Shinyanga, Kama hivyo ndivyo ile Azma ya kuikwamua hii nchi toka Mkoloni mweusi juhudi na kasi zake ziongezeke maardufu. Kwani Shinyanga ikitowa Almasi toka vita vya Mironge Mgao wa mkoa uko wapi? au hakuna mpango huo Wazee wa Vijisenti wanajengea mahekalu DSM? AIBU GANI!!!
Watanzania wenzangu, kwa nini hatutaki kuelewa MAENDELEO YA WATANZANIA YATALETWA NA WATANZANIA.
Maendeleo ya Kinondoni yataletwa na Wana Kinondoni, sio Mbunge.
07/08/2010
Picha na maelezo kwa hisani ya Wavuti.com
Takriban miaka Hamsini tangu tujiite kuwa Huru (nusu karine inaingia) Angalia hiyo picha naamini itakukumbusha nyingi ulizoziona hapa na kwengineko. Zifikirie Huduma za Afya, Elimu, Usafiri nk.
Mfikirie Raisi wako na Mawaziri wake, wafikirie Wabunge wetu na Maafisa wakuu wa serekali, mkumbuke Benjamin Mkapa, Chenge, Lowasa, Ndilu na wale wa aina yao, halafu ingalie tena hii Picha. Najua hatuko sawa na wala hatuwezi kuwa sawa, lakini ni wazi kuna Mstari unakosekana mahali, mstari wa Uwiano umekiukwa vibaya, tena vibaya sana, kwa Waumini wa Dini wanaweza kudai kuwa tumo katika Kukufuru, na ndio maana nauliza MAPAMBANO YANAANZAAAA? AU YANAENDELEAAAAA!!!!!! 50 YEARS ON....
Shy-Rose Bhanji, Handeni, Tanga
Ni jambo la heri kutembelea watu katika maeneo ya vijijini ili kupata uhalisia wa maisha huko kwa ajili ya kujipanga vyema na kuwa sauti yao katika kufikisha mahitaji yao katika ngazi husika za uongozi, pia kupanga na kuandaa mikakati ya kuwakwamua katika mazingira magumu ili nao wajisikie kuwa sehemu ya jamii inayofurahia huduma muhimu kama vile maji, umeme, barabara, shule nk.
Hongera Shy-Rose.
at least wana madawati