mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Kuna jamaa yule mwenye jezi ya Yanga alivyotolewa nilitegemea watu wangelia machozi ya furaha lakini wapi,...watu walikuwa kama wanshangalia movie,hakuna hisia kwenye nyuso zao,walishangilia utadhani wako mpirani wakati jamaa alikuwa katikati ya kifo na mauti,...Wanatamani lile zari lingewatokea wao wakawa wanahojiwa na vyombo vya habari,wasichokijua jamaa kaishapoteza mtaji na anaenda kuanza upya,huenda akapitia pagumu kurudi kama mwanzo
Kuna wale graduate mwaka wa nane huu hawana kazi wako kwa shemeji,wanalala sebuleni ,hawa nao wanatamani wangedondokewa na kifusi wafe.
Kuna wale wenye madeni mpaka nyumba inataka kuuzwa na benki na hawajui watalipaje madeni au watoto watalala wapi nyumba ikiuzwa...
Kuna wale wanaumwa magonjwa hatari kama kupooza au kansa,maumivu wanayopata,wameshakata tamaa ya kuishi
Tuwaombee watu hawa