Si bidii wala juhudi ziletazo mafanikio

Si bidii wala juhudi ziletazo mafanikio

Mnyakyusa5000

Member
Joined
Sep 21, 2021
Posts
83
Reaction score
136
Tumefundishwa vibaya. Tangu tukiwa watoto tumeambiwa kufanya kazi kwa bidii huleta mafanikio. Tumehakikishiwa kuwa hakuna njia nyingine isipokuwa hii.

Sasa tumekua. Tumeingia katika shughuli za uzalishaji na mahusiano. Mambo haya mawili yaani uzalishaji mali na mahusiano yamekuwa mzigo mzito usiohimilika. Wengi wetu hatujafanikiwa kuhimili changamoto nyingi zitokanazo na mahitaji yanayotegemea vitu hivi.

Juhudi zetu hazizai matunda. Tunaamka asubuhi na mapema. Tunalala usiku wa manane. Hakuna kitu. Hatutoboi. Mahusiano hayawi bora wala hali zetu za kiuchumi.

Sasa ni muda wa kujiuliza. Je, tulielekezwa jambo sahihi? Ni kweli kuwa bidii na juhudi ndio njia pekee ya mafanikio? Mbona hatufanikiwi? Sisi sio wavivu. Sisi hatuchagui kazi. Inakuwaje?

Ukweli ni kuwa si sahihi kwamba bidii na juhudi huleta mafanikio. Sio kweli. Mafanikio hayaji kwa kufanya kazi kwa bidii bali kufanya kazi kwa furaha.

Mwanazuoni mashughuli aitwae Napoleon Hill ameandika katika moja ya vitabu vyake juu ya aina kumi na mbili za mafanikio. Anasema kuwa mafanikio ni: kuwa na akili tulivu, afya njema, mahusiano mema, kuwa huru dhidi ya hofu, kuwa na matumaini, kuwa na imani, ushirikiano, upendo, utayari wa kujifunza, nidhamu, kuwaelewa watu na kuwa na pesa.

Aina zote hizo za mafanikio hazipatikani kwa kuwa na bidii au juhudi isipokuwa hupatikana pale mtu anapoamua kuwa na furaha wakati wote.

Furaha tunayoizungumzia ni ile furaha ya asili. Furaha isiyotegemea mtu au kitu chochote. Furaha ambayo mtu huwa nayo bila sababu.

Tujifunze kufurahi wakati wote. Inalipa. Jaribu uone muujiza. Tabasamu kwa furaha wakati wote. Ongea na watu kwa furaha. Ishi nao kwa furaha. Fanya kazi kwa furaha. Furahi bila sababu yoyote. Wewe furahi tu. Furahi jua likiwaka. Furahi mvua ikinyesha. Fanya kila kitu unachopaswa kukifanya ukiwa na furaha uone jinsi aina mojamoja ya mafanikio itakavyokuja upande wako.
 
Neno zuri sana tena la faraja! Asante Mnyakyusa5000
Hakika linafariji sana...
Hapo kwenye muwa hur dhidi ya hofu kwangu ndio changamoto sana.

Sio kwamba mambo ni mabaya kihivyo ila always huwa naogopa sana sometimes about future...what will happen? Leo niko fine sawa but mambo yatakuwa sawa hiv for next few year?? For me...for my kids... yan hapo sijui natokaje!
 
Mafanikio ni namna mtu anavyotazama, kwa wengine mafanikio ni kupata elimu kubwa, wengine huamini mafanikio ni ukwasi wa fedha na mali(hawa ndio wengi) na wengine huamini mafanikio ni kupata mpenzi alie bora kwa vigezo vyake na kadhalika.

Kuu ni kuwa mafanikio bado yanahitaji maarifa ya kweli, kuchangamana na watu(connection) pamoja na juhudi. Bila juhudi na jitihada ni wazi uvivu hutamalaki mbele ya mtu na hivyo mwenye kuhitaji mafanikio sio tu yule alyekaa akitaraji kuwa eti ipo siku atapata, bali mwenye kuhitaji mafanikio ni lazima huyafanyia kazi mambo hayo makuu matatu ili kuweza kutengeneza output ya anachokihitaji. Waslam (Huu ni mtazamo binafsi).
 
Hakika linafariji sana...
Hapo kwenye muwa hur dhidi ya hofu kwangu ndio changamoto sana.

Sio kwamba mambo ni mabaya kihivyo ila always huwa naogopa sana sometimes about future...what will happen? Leo niko fine sawa but mambo yatakuwa sawa hiv for next few year?? For me...for my kids... yan hapo sijui natokaje!
Jifunze tu kutulia..hatua kwa hatua..utaweza..jitulize kika wakati unapoanza kuhofu..
 
Mafanikio bila maendeleo ni Sawa na ndege mwenye bawa moja.

Mafanikio ni siri. Na maendeleo ni.........

Tafadhali nijuze siri ya mafanikio yako nami nitoboe

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Hakika linafariji sana...
Hapo kwenye muwa hur dhidi ya hofu kwangu ndio changamoto sana.

Sio kwamba mambo ni mabaya kihivyo ila always huwa naogopa sana sometimes about future...what will happen? Leo niko fine sawa but mambo yatakuwa sawa hiv for next few year?? For me...for my kids... yan hapo sijui natokaje!
Jifunze tu kutulia..hatua kwa hatua..utaweza..jitulize kika wakati unapoanza kuhofu
Mafanikio bila maendeleo ni Sawa na ndege mwenye bawa moja.

Mafanikio ni siri. Na maendeleo ni.........

Tafadhali nijuze siri ya mafanikio yako nami nitoboe

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
Siri ni kuwa na amani na furaha wakati wrote...jifunze kupuuza mambo yote yanayokunyima ivo vitu viwili...sio rahisi mwanzoni lakini inawezekana ukijizoesha
 
Back
Top Bottom