Si Haba, Utawala wa Malinzi na mafanikio dhahiri ya soka

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Utawala wa Jamal Malinzi umekuwa ukipokea shutuma nyingi kutoka pande mbalimbali za wadau wa soka. Mimi pia ni mmoja wa wakosoaji wake. Watu wengi tumekuwa tukihoji uwezo wake kiuongozi, uadilifu na umakini wake na wasaidizi wake katika shughuli ya usimamizi wa mchezo huu pendwa kuliko yote hapa nchini.

Mambo kama kashfa za rushwa na upangaji matokeo, tuhuma za ukabila, matumizi mabaya ya fedha, ubabe kwa kufungia wapinzani wake, na mengine yanayofanana na haya ndio yamekuwa mambo ambayo utawala huu umekuwa ukihusishwa nayo. Ilifikia watu kuona Malinzi na wenzake wameturudisha kipindi cha FAT ya akina Ndolanga na Rage.

Lakini katikati ya haya yote kuna kitu kiko dhahiri, nacho ni mafanikio ya kisoka katika miaka hii ya TFF chini ya Malinzi kuliko vipindi vingi tu huko nyuma! Na ili wadau tutende haki ni lazima tuzungumzie mambo haya kwa nia ya ku -acknowledge badala ya kukosoa tu sikuzote. Wakati tunaendelea kumkosoa ili kumtia spidi gavana, Malinzi ametujibu kupitia mafanikio yafuatayo, tena kwa mpigo;

1. Azam kuwa bingwa wa vilabu vya Afrika Mashariki na Kati (KAGAME)
2. Yanga kuwa timu pekee ktk eneo la ukanda wa CECAFA kucheza makundi ya kombe la
shirikisho la CAF.
3. Kilimanjaro Queens kutwaa kibabe ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
4. Serengeti Boys kukaribia kufuzu kushiriki fainali za vijana za CAF.
5. Kuendelea kuimarika kwa ushindani wa Ligi ya VPL na kupungua kwa malalamiko dhidi ya waamuzi.

Ni ukweli si mafanikio ya maana sana, lakini kwa nchi ambayo tumekuwa tukiambulia patupu karibu kila michuano ya soka tunayoshiriki, angalau kuna kitu kinaonekana hasa tunapoanza kuwa wababe kwa wanyonge wenzetu wa CECAFA. Hongera Malinzi.
 
Hayo mafanikio yeye amechangia kitu gani? Mbona hujaeleza kuhusu kuporomoka kwa Taifa Stars kwenye viwango vya FIFA? Au ameamua kuelekeza nguvu kwenye Yanga/azam/ Serengeti na Kilimanjaro Queens? Malinzi hana uwezo wa kuleta mafanikio kwenye soka letu, ni mroho wa madaraka na hana vision kabisa.
 
Umelipwa how much kuleta huu Uzi?
 


Hizi njaa zingine hata hazifai..
Jitu limeboronga,soka halina mvuto,timu ya taifa kila siku inafungwa,yanga imetolewa kombe la shirikisho,migogoro,ratiba za hovyo,ratiba zinahairishwa timu ikacheze kikombe,upangaji wa matokeo,wadhamini wamekimbia,ukabila,rushwa,rais hana visheni,kombe la coca cola sijui limefia wapi alafu anatuma mtu aje amsifie hapa jamii forum wakati yeye kitambo akaunti yake hapa JF ameikacha. Au we muhaya mkuu?
 
 
Nimejituma mwenyewe, na wewe umetumwa na nani kuuliza swali la kipuuzi?

Shida ya Malinzi hataki kukosolewa,yupo kama jamaa fulani hivi siku hizi anakaa pale jirani na feri,yaani ukimkosoa tu anadhani umetumwa na unataka cheo chake,halafu hapendi kusikiliza maoni ya wadau yeye anaamini wale wachache aliowaweka kumshauri kitu ambacho si sawa,ila namsifu jinsi anavyoitunza Serengeti Boys au kwa ujumla timu za soka ya vijana anafanya vizuri,ila kwenye timu ya taifa ya wanawake hapo inabidi ashirikiane sana na chama cha soka la wanawake ili kuihudumia timu hii,ningekuwa malinzi mkazo wangu nungeweka kwenye soka la vijana na wanawake kwani ndizo angalau hapa kwetu zina historia ya kufanya vizuri kuliko hao wakubwa ambao kila mwaka ni aibu tu.
 

Nakubaliana na wewe. Na pia hongera, wewe ndio umejadili hoja tangu mada ilipowekwa mezani.

Taifa zima tunapaswa kuweka nguvu kwenye mashindano na timu za vijana. Kwa mfano ilitakiwa saa hizi Ngorongoro Heroes na Under 23 ziwe ziko kwenye maandalizi na kucheza mechi za kirafiki. Utasikia bado wiki 2 ya mashindano, ndio maandalizi yanaanza. Hata mpira wa wanawake tunaweza kufanya vizuri zaidi kuliko Taifa Stars ya sasa
 

Soka la vijana ndio msingi wa mpira sehemu yoyote duniani,nadhani na yeye alilifahamu hilo ndo maana kwa kiasi fulani amelitilia mkazo,japo ni vigumu sana kupata wadau na wafadhili wa kulisapoti,kwani watu wengi wanapenda kuona matokeo ya haraka,lakini mimi namshauri aendelee na juhudi hizi hizi za kuzisapoti timu zote za vijana bila kuisahau timu ya wanawake muda si mrefu matunda yataonekana na wanaomsema watabaki hawana hoja,isipokuwa awe mvumilivu asipende kufungia watu kwani ataonekana kama ni mtu wa visasi na vinyongo kitu sio sawa,ajitahidi kuwa fair na hata wakati mwingine kujifanya mjinga kwani huku kwenye soka kuna maneno ya shombo sana yambidi atambue hilo,kwenye soka ndio mahali pekee mtu lofa hana hela lakini anamkoromea tajiri anayeitunza timu kwa pesa yake.
 
Umeichaka ile ID yako inayotambulika nini? umeamua kuja kivingine
 

Taifa litaweka vipi nguvu wakati uongozi wa Malinzi na watu wake wamekaa kiupigaji tu.Hawana mipango yoyote kumbuka soka sehemu kubwa linaendesha chama cha mpira.Mpaka Malinzi atoke pale TFF ndio tunaweza kuona mabadiliko ya hayo unayoyasema.Viongozi kama Tenga alikuwa na vision na laiweka msisitizo katika soka la vijana leo hii tuna kina Samatta.Timu ya Taifa ilkuwa ya 85 katika viwango vya FIFA hivi sasa ni ya 132




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…