Ni kweli bado madudu ni mengi lakini niseme kwa maandalizi ya Serengeti boys, TFF imejitahidi sana. Tuwe wakweli katika hili, ni sawa na mwanafunzi aliyepata swali moja vizuri kati ya kumi aliyokosea. Sidhani kama ni sahihi kumkosesha hata hilo moja.
Lakini pili, hatuwezi kuachia maendeleo ya soka kwa TFF pekee. Hapo ndio tunaposea. Mpira una wadau wengi, ikiwemo serikali kama mdau mkuu, vilabu vya soka, vyombo vya habari, wadhamini, mashabiki n.k. Suala la maendeleo ya timu za vijana na wanawake sio la kuachia TFF pekee. Tumejaribu hivyo miaka mingi imeshindikana. Kinachofanywa na Azam kwa mfano ndio kinapaswa kuigwa na vilabu vingine . Ndio maana nasema lazima taifa zima lishiriki.[/QUOTE]