LGE2024 Si jukumu la vyama vya siasa kusimamia uandikishaji wa wapiga kura na uwepo wa mawakala wa vyama kwenye zoezi

LGE2024 Si jukumu la vyama vya siasa kusimamia uandikishaji wa wapiga kura na uwepo wa mawakala wa vyama kwenye zoezi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Unapokwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura hapaswi kutaja chama chako cha siasa na huu sio wakati wa kampeni.

Ni makosa makubwa kwa vyama vya siasa kuwa wasimamizi kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura. Kwenye daftari la wapiga kura hatuandikishi CCM, CHADEMA, etc bali tunaandikisha mtanzania mwenye sifa za kupiga kura.

Kumbukumbu za walioandikishwa hazitunzwi na vyama vya siasa bali na Tume huru ya uchaguzi.

Daftari la wapiga kura sio la chama fulani ni mali ya tume ya uchaguzi.

Uwakala wa vyama kwenye zoezi la wapiga kura ni jambo batili kabisa na halina mantiki yoyote na ni kiashiria kikubwa cha uvunjifu wa demokrasia.

Mtu hapaswi kuandikishwa kwa sababu eti atapigia kura CCM au CHADEMA! Inashangaza mno kuona jambo hili batili kabisa likifanywa na kusimamiwa kana kwamba ni jambo sahihi.
 
Unapokwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura hapaswi kutaja chama chako cha siasa na huu sio wakati wa kampeni.

Ni makosa makubwa kwa vyama vya siasa kuwa wasimamizi kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura. Kwenye daftari la wapiga kura hatuandikishi CCM, CHADEMA, etc bali tunaandikisha mtanzania mwenye sifa za kupiga kura.

Kumbukumbu za walioandikishwa hazitunzwi na vyama vya siasa bali na Tume huru ya uchaguzi.

Daftari la wapiga kura sio la chama fulani ni mali ya tume ya uchaguzi.

Uwakala wa vyama kwenye zoezi la wapiga kura ni jambo batili kabisa na halina mantiki yoyote na ni kiashiria kikubwa cha uvunjifu wa demokrasia.

Mtu hapaswi kuandikishwa kwa sababu eti atapigia kura CCM au CHADEMA! Inashangaza mno kuona jambo hili batili kabisa likifanywa na kusimamiwa kana kwamba ni jambo sahihi!
Mimi mwenyewe nashangaa ccm na chadema na vyama vyote tulivyo navyo ni jamii ya watu wapumbavu haswa awajui nini ni nini...
Kuna hiki kitu nasema usiku na mchana ila hakuna mwenye akili anaye jua kwanini nakisema sana

👉 NI KOSA KUBWA SANA WANASIASA KUWA WAPIGA KURA KWENYE CHAGUZI KUU YAANI KURA YA URAIS ...UBUNGE...UDIWANI.💥💥💥
Hii kanuni moja tu ingetatua asilimia 80% ya matatizo ambayo tunapitia ....ningekuwa na muda ningeandika faida elfu 10 za kuzuia wana siasa kuwa wapiga kura ....wapo watu wanasema kenya ina katiba nzuri ! Je kwenye katiba ya kenya kuna kanuni hii ya kuzuia wana siasa kuwa wapiga kura ? Kama hakuna ndiyo sababu mnaona kenya bado wana matatizo chungu mzima kwenye nchi yao yanayo husu siasa na uongozi ....kamwe katiba hata ikiwa nzuri namna gani hila ikaruhusu wanasiasa kuwa wapiga kura basi hiyo ni katiba mbovu natudia tena ni katiba mbovu narudia mara ya 3 ni katiba mbovu ....sasa jiulizeni ni nini kitatokea kama wana siasa watazuiwa kikatiba kupiga kura? Hapo mtagundua faida maelfu kama mnayo akili kubwa ya kupambanua mambo .....pia mfumo huo ungepunguza ukabira kwa mataifa kama kenya
 
ndio sababu watu wengi hawaendi kujiandikisha mpaka wanatumia matamasha na ushawishi mkubwa matangazo mengi lakini watu walio wengi hawataki kwenda watu hawataki kuulizwa wewe ni ccm au chadema? ukishajiandikisha unakuwa kama umeshapiga kura kwenye chama fulani.
 
Mawakala ni muhimu katika kutambua watu wanoishi katika mazingira Yao. Si wanasema waandishi ni CCM? Mawakala wasipokuwepo inadaiwa waandishi wataandika majina hewa,wataandika watu wamaeneo tofauti au wanaweza kuandika hata watoto wadogo. Wawepo tu ili waanze kujiridhisha na zoezi kabla ya uchaguzi kuepuka malalamiko.
 
Mimi niliposikia suala la uwepo wa mawakala wa vyama vituoni, nilidhani ni kwenye zoezi la upigaji kura siku ya uchaguzi..... sikujipa muda wa kutafakari vema.

Kama ni kweli hayo ndo yanayofanyika kwenye kujiandikisha basi ni ukhanithi uliokubuhu.
 
Unapokwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura hapaswi kutaja chama chako cha siasa na huu sio wakati wa kampeni.

Ni makosa makubwa kwa vyama vya siasa kuwa wasimamizi kwenye zoezi la uandikishaji wa wapiga kura. Kwenye daftari la wapiga kura hatuandikishi CCM, CHADEMA, etc bali tunaandikisha mtanzania mwenye sifa za kupiga kura.

Kumbukumbu za walioandikishwa hazitunzwi na vyama vya siasa bali na Tume huru ya uchaguzi.

Daftari la wapiga kura sio la chama fulani ni mali ya tume ya uchaguzi.

Uwakala wa vyama kwenye zoezi la wapiga kura ni jambo batili kabisa na halina mantiki yoyote na ni kiashiria kikubwa cha uvunjifu wa demokrasia.

Mtu hapaswi kuandikishwa kwa sababu eti atapigia kura CCM au CHADEMA! Inashangaza mno kuona jambo hili batili kabisa likifanywa na kusimamiwa kana kwamba ni jambo sahihi!
Bro una akili sawasawa?
Wakati mama Harris Marekani akizunguka kutafuta wapiga kura wenye asili ya kiafrika ili wampigie kura, na Trumpanaenda states za mabwanyenye ili wampe kura, wewe unatoa upoyoyo kwenye jamvi?
 
Tunapoteza pesa kuchagua watu ambao hata kujiudumia viatu na ndala tu hawawezi halafu tunatumia mabilioni kuandaa chaguzi

Wagombea wenyewe thinking capacity yao ukiwa chini halafu tunategemea maendeleo ningekuwa Mimi nateua wagomea kigezo Cha kwanza kumiliki nyumba yenye umeme na gari yako nzuri ndo unakuwa mwenyekiti.

Ccm utumia wajinga ili kuendelea kuwa madarakani
 
ni takwa la kisheria katika sheria ya uchaguzi... ccm wameibadilisha kuwa fursa
 
ningekuwa na muda ningeandika faida elfu 10 za kuzuia wana siasa kuwa wapiga kura ..
Hoja yako haijaeleweka. Kabla ya kuandika ulipaswa kujiuliza na kujipatia maswali haya:-
1. Mwanasiasa ni nani?
2. Diwani, mbunge na rais kabla ya kuchaguliwa kushika nafasi hizo za kisiasa walikuwa wanasiasa?
3. Mwananchi wa kawaida anayekwenda kujiandikisha ni mwanasiasa?
 
ULICHO ANDIKA KINAONYESHA UWEZO WAKO MDOGO SANA WA KUELEWA ...TULIZA AKILI ..KISHA RUDIA KUSOMA KWA KUTUMIA AKILI UTAJUA NILICHO MAANISHA ...UKIWEZA KUJUA NILICHO MAANISHA JUA UMEANZA KUPONA UNGONJWA WAUPUMBAVU ...MAANA KAMWE MTU MPUMBAVU AWEZI KUELEWA MAMBO MAKUU KAMA HAYA NILIYO YA ANDIKA .
Kwa kifupi ni hatari sana vyama vya siasa kuwa na mamilioni ya wanachama wa kazi gani ? Zaidi nchi itangia kwenye ushabiki wa kisiasa kama mpira...wanasiasa wakiwa siyo wapiga kura mara moja vyama vitaanza kutumikia wananchi kama wananchi siyo kutumikia wanachama wao ...imefika wakati tunakuwa kama burundi uwezi kupata kazi serikalini kama siyo mwanasiasa wa chama tawala ..pia uwezi kupata cheo kikubwa popote kama siyo mwanachama wa chama tawala...leo hii tumefikia hatua ya serikali kutumikia wanachama wa ccm badala ya kutumikia taifa ...wao ndiyo wanapewa na kupeana mikopo rafiki walipe wasilipe hakuna kufilisiwa je hiyo mikopo.kwanini itolewe kisiasa wakati ccm na serikali yake ni chama tawala kwa watz wote ....kuzuia wanasiasa kuwa wapiga kura kutafanya vyama viwe na wanachama wachache makini na kuwatumikia wananchi pasipo kuangalia chama maana wapigakura wasingekuwa wanasiasa....TUMIENI AKILI
 
ULICHO ANDIKA KINAONYESHA UWEZO WAKO MDOGO SANA WA KUELEWA ...TULIZA AKILI ..
Kichaa huwa hajijui kuwa ni kichaa. Umeegesha akili yako yote kwenye matusi badala ya kupangua hoja. Kama unatumia vileo usiandike hoja mitandaoni.
 
Kichaa huwa hajijui kuwa ni kichaa. Umeegesha akili yako yote kwenye matusi badala ya kupangua hoja. Kama unatumia vileo usiandike hoja mitandaoni.
I NEVER UNDERESTIMATE THE STUPIDITY OF YOUR STUPID ...HOJA GANI ULIYO ULIZA.
 
Hakuna uchaguzi hapo ni kupoteza muda tu.

Upinzani hamjufunzi tu?
IMG-20241017-WA0003.jpg
 
Ni muhimu kuelimisha watu wakuelewe kuliko kulazimisha watu ueleweke!!

Tatizo letu Kama nchi tuna uhaba wa watu waaminifu. Suala la uandikishaji lilipaswa kusimamiwa na Tume ya uchaguzi, then majina yanabandikwa na kuwekewa pingamizi yenye utata.

Suala la kuweka wakala wa vyama kwenye kuandikisha ni matumizi mabaya ya muda wa raia wake. Tume haiaminiki, serikali nayo haiamiki kwa kuwa njia iliyotumika kushika madaraka ni za kiulaghai!!

Kumwaamini kiongozi laghai wewe utakuwa na matatizo makubwa Sana ya akili. Kifupi wewe ni marehemu!!

WAY FORWARD
Tujenge mifumo isiyoingiliana!!
Serikali,mahakama,bunge,Tume ya uchaguzi, ofisi ya CAG. Sheria mama(katiba) itaje kuwa kila mhimili utajisimamia kwa mjibu wa kanuni!!

Kukiwa na utendaji mbaya wa kiongozi kuwe na uondoaji usiotilia shaka.

Upatikanaji
wa Watendaji wa TUME ukiwa wa haki na wa WAZI hakuna atakayetilia shaka.

Mashaka yanapoanzia kwa mkuu wa Tume ya uchaguzi mpaka msimamizi wa kituo suala la wakala haliepukiki!!

Uwe na akili usiwe na akili huo ukweli unabaki hivo
 
Back
Top Bottom