Si kila anayetoka Kagera ni Mhaya

Si kila anayetoka Kagera ni Mhaya

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
KAGERA NI MUHAYA Turejee Historia. Wahaya ni nani? Jina Wahaya lilianza kutumika lini? Jina Wahaya linatokana na nomino IHAYA. Huu ni mwambao wa Ziwa Lweru.

Hadi ujio wa Wazungu lilimaanisha mwambao wa ziwa hilo sehemu za sasa Kyamutwara na Maruku. Ihaya lilikuwa ni eneo la vijiji vya wavuvi. Kwahiyo neno Wahaya lilimaanisha wavuvi. Katika kitabu cha Historia ya Bukoba, Hans Cory anasema jina Muhaya lilikuwa ni tusi dogo maana wavuvi hawakuwa na mahali pa kudumu pa kuishi na hawakuwa na mali ya kudumu.

Neno Ihaya halikuishia Kyamutwara na Maruku. Ihangiro ya zamani, uligawanyika sehemu mbili: Migongo na Omwihaya.

Kwa hiyo matumizi ya jina Wahaya yalienea hadi Ihangiro. Rekodi za wapelelezi wa Kizungu zinataja jina Buhaya. Omukama Rumanyika Orugundu alimwambia Speke: Mashariki mwa Karagwe kando ya ziwa kunaitwa BUHAYA ni maarufu kwa kilimo cha mibuni na pembe za ndovu. Mwisho wa kunukuu.

Katika vitabu vingine kama vile Victoria Nyanza, Karagwe ina sura yake na eneo lote Mashariki ya Karagwe wanaliita Kiziba.

Athari hiyo bado ipo Baganda huita Wahaya wote Baziba Jina Wahaya linaendana na jina jingine BUKOBA. Bukoba ni sehemu ya ukoo wa ABAKOBA. Ni pale kastamu.

Kwa kweli Bukoba kama eneo walikaa Wavuvi, Abahaya. Kuenea kwa matumizi ya majina Bukoba na Wahaya kuliambana na uvamizi wa wakoloni.

Wajermani walilipanua kujumuisha mji wa Bukoba, baadaye tawala zote za kando ya ziwa. Kwa wakati huo Karagwe haikujumuishwa. Na hata Omukama Ntare wa Karagwe walipomnyonga. Karagwe iliwekwa kwenye usimamizi wa Omukama Kahigi wa Kihanja ila ikabaki inajitegemea."
 
Kwahiyo ndani ya Wilaya ya Kyerwa hakuna mipaka ya nchi hizo mbili?
Kiongozi Mimi Nilipita Sijaishi Huko
Sijajua Kama Kuna Mipaka Hiyo

Ila Nilipita Pori La Burigi Chato National Park
Siyo Rahisi Kuwa Na Mipaka Hiyo
Bila Shaka Lazima Itakuwa Nchi Ya Uganda, Rwanda, Burundi. Ukweli Nimetembea Wilaya Zote Za Mkoa Wa Kagera Tena Nilitokea Biharamulo, Muleba, Mpaka Misenyi
Ndiyo Unakwenda Karagwe
 
Mkuu, ninatamani sana kufika Wilaya moja inaitwa Kyerwa. Ninasikia katika Wilaya hiyo moja kuna mipaka ya nchi mbili za Uganda na Rwanda?
Pia ufike na Ngara uone eneo maarufu kama mafiga matatu kwa wenyeji wa huko, ni mpaka unaotenganisha Tanzania, Burundi na Rwanda. Kwa jinsi palivyo ni kama mafiga japo mto kagera ndio umetenganisha Rwanda na Tanzania, huku Burundi na Tanzania zikitenganishwa na bonde.
 
Mkuu ramani yako imekaa vibaya, baada ya kyerwa ni Karagwe, halafu Ngara rusumo.
Sio karagwe, kyerwa, Ngara rusumo.

Karagwe imepakana na Rwanda wakati kyerwa ni Rwanda na Uganda.
Mkuu Mimi Nilitokea Misenyi, Halafu Nikaenda Karagwe
Hapo Sasa Nikakatiza Lile Pori Mpaka Rusumo
 
Mkuu Mimi Nilitokea Misenyi, Halafu Nikaenda Karagwe
Hapo Sasa Nikakatiza Lile Pori Mpaka Rusumo
Missenyi imepakana na kyerwa na bukoba, ukitoka Missenyi utaenda kyerwa halafu Karagwe.
 
Back
Top Bottom