"Bongolander, post: 31861380, member: 3997"]
Mimi sioni kama ni vibaya kumkosoa Magufuli.
Hata yeye mwenyewe huwa anajikosoa, na pale anapoona amekosea anajaribu kubadilisha.
Tupe mfano mmoja ili wote tusome ukurasa ule ule ''same page''
Uongozi wa kufuata sheria na unaoheshimu katiba kweli unafaa sana, kama haufanyi usanii. Nadhani wengi tunapenda tufike huko, ambako bado hatuajafika. Iwe ni sababu ya kuwa na mashaka na katiba yenyewe, au iwe ni sababu ya mianya ndani ya katiba, au kukosa muundo imara wa kulinda na kutetea katiba. Tatizo langu mimi kwenye issue hii ni kuwa, kuna wale ambao wanatumia katiba kutuibia au kutufanya tuwe duni, na wengine wanatumia katiba kwa maslahi binafasi na sio maslahi makuu ya taifa.
Katiba inayotoa fursa ya kuiba, kutufanya tuwe duni, kutumika kwa masilahi binafsi siyo katiba inayofaa.
Ironically, katiba inatakiwa ilinde umma dhidi ya mambo hayo.
Suluhu si kuiacha ibaki kama katiba ili tuonekane tuna katiba.
Fikra hizo ndiyo ' real kichwa cha panzi''.
Una kidonda mguuni badala ya kutafuta tiba unakiacha kioze kwasababu tu upo bize kupanda mnazi ili upate madafu. Hapo ndipo ''kichwa cha panzi 'kilipo.
Suluhu ni kukaa chini na kutengeneza katiba inayokwendana na wakati , matakwa na mahitaji ya nyakati. Hapa unaunga mkono hoja yangu kuwa hatuna mwelekeo kwasababu hatuna mwongozo ambao ni KATIBA.
Hapa ni wote wana CCM na wapinzani.
Mkuu unaonekana kuwa obsessed sana na Wapinzani.
Hivi kweli unaweza ku-equate wapinzani na chama tawala!
Hawa wapinzani hawajawahi kutawala nchi hii hata kwa masaa machache, wapi unapata ushahidi wa kusema wanatumia katiba kutuibia, kutifanya tuwe duni na kwa masilahi yao?
Kwanini unatafuta balance hata kwa jambo lilowazi kama hili!
Hebu nionyeshe ni kwa namna gani Wapinzani wametumia katiba kutuibia, kutufanya tuwe duni au kwa masilahi yao. Kuna uwezekano kabisa lipo jambo nisilo lijua. Tafadhali tusaidi
Lakini kuna wengine ambao ndio nawalaani zaidi, wanapenda kujionyesha (kwa nchi za magharibi) kuwa wanafuata katiba lakini gharama yake kwa taifa ni kubwa, ni kama tunagharamia mchezo wao.
Kama tunatumia katiba kufanya uchaguzi, kupata viongozi, kuwaapisha viongozi na kuunda serikali kuna ubaya gani kuonyesha kuwa sisi ni nchi yenye kufuata katiba tuliyo nayo?
Kwangu mimi binafasi maendeleo ni kitu cha kwanza na cha msingi kabisa.
Hili nalirudia kila mara.
Watanzania hawaelewi kabisa kuwa Maendeleo si kontena la bidhaa linalotengenezwa au kuagizwa kupitia bandari ya Dar es Salaam.
Maendeleo ni mchakato wa fikra na matendo.
Huwezi kuwa na maendeleo bila mawazo na kama huwezi kuyafanyia kazi mawazo hayo.
Lakini si hivyo tu, mawazo ya kufanyia kazi yanahitaji nidhamu.
Nidhamu si kibuyu cha pombe ya ndaza, ni utaratibu maalumu unaotoa fursa kimpangilio.
Hivyo nidhamu lazima iambatane na sheria ambayo chimbuko lake ni mkusanyiko wa mawazo na mipango katika mfumo wa katiba.
Kitu cha kwanza hakiwezi kuwa maendeleo, lakini matokeo ya mpangilio wa fira, matendo na nidhamu ndiyo unazaa kitu kiitwacho maendeleo
MImi binafsi kutokana na kiwango cha maendeleo ya nchi, nisingependa kitu chochote kinizuie kuleta maendeleo ya nchi, iwe katiba, iwe chama au hali yoyote.
Katiba inayokupa haki ya kuleta maendeleo inawezaje kuwa kikwazo tena? I mean hapa sielewi kabisa
Lakini nachukia watu wanaojaribu kutumainisha kuwa JPM anavunja katiba as if Mwalimu, Mzee Ruksa, Mkapa na JK hawakufanya hivyo. Ukiangalia kuna cases nyingi tu ziliwahi hata kufikishwa mahakani kuhusu ukiukaji wa katiba. That is not the issue for Tanzanians. Issue kwa sasa ni maendeleo.
Maana ya uongozi, ni kupanga, kuonyesha na kufanya yaliyo bora.
Mkuu utetezi kuwa Mwl, AH, BWM walifanya abcd hivyo ni halali kufanya tu ni mawazo hafifu na ya hatari sana na sijui kama kuna mtu mwingine anaweza kukuelewa,SIJUI
Huwezi kulinganisha ubaya kwa ubaya hata siku moja.usisahau kipimo cha uzuri ni ubaya.
Sasa kama unalinganisha ubaya na ubaya uzuri utaupata wapi?
Tena ukimlinganisha Mwalimu na viongozi wote waliofuata , Mwl ana advantage kubwa sana
Mwalimu hakuwa na template, kila kitu kilikuwa cha kwanza na kigeni
Sasa kiongozi akiwa na template halafu akafanya sawa au vibaya kuliko Mwl, unatueleza nini?