Si kila unachokitamani kitakufaa

Si kila unachokitamani kitakufaa

Chegge

Senior Member
Joined
Mar 18, 2026
Posts
159
Reaction score
3
Unajisikiaje pale ambapo ulikuwa mke wa mtu una nyumba yako, una heshima yako na unatambulika kama mke wa mtu, lakini kwa sababu ya maamuzi yako mwenyewe na upumbavu wa kutokujua unachokitafuta, unajikuta umeachika na mwisho wake unageuka kuwa mchepuko wa mwanaume mwingine?

Yaani jana ulikuwa unapewa nafasi ya mke, leo unapewa nafasi ya kujificha! Jana ulikuwa unahojiwa kuhusu matumizi ya nyumbani, leo unauliza, “Mbona hujapokea simu zangu?” Jana ulikuwa unajua unalala kwa mume wako, leo unasubiri ujumbe wa mwanaume ambaye hata ukimtafuta Jumapili anakwambia yupo na familia!

Jiulize, je, hiyo ndiyo ilikuwa thamani ya uhuru uliokuwa unautafuta? Wakati mwingine mtu anaweza kuharibu maisha yake mwenyewe akidhani anatafuta furaha, kumbe anabadilisha nafasi ya heshima na amani kwa nafasi ya mashaka na kujificha.

Kumbuka, si kila unachokitamani ndicho kitakachokufaa. Kabla hujaharibu ulicho nacho kwa sababu ya hisia za muda mfupi, jiulize utakuwa umepata nini na umepoteza nini. Maana si kila kutoka kwenye ndoa ni kwenda kwenye maisha bora; wakati mwingine unatoka kuwa mke wa mtu na kuingia kwenye foleni ya kusubiri kuitwa.
 
Back
Top Bottom