Si kwa ubaya lakini naona anguko la Harmonize

Si kwa ubaya lakini naona anguko la Harmonize

brownboy

Senior Member
Joined
Jun 10, 2023
Posts
103
Reaction score
278
Nyimbo anazotoa hazina mvuto tena na hazishiki number one kwenye platform yoyote mpaka boomplay ambayo inaonewa mpaka na maunderground kwa kushika number one trending.

Watu wanamkimbia kwenye show. Kondegang ndo hivyo imekufa plus kiki zake ndo hivyo hazihit. Hali ikiendelea hivi basi hatutomsikia tena Harmonize.
 
Nje ya topic kidogo. Huwa sielewi mtu akisema on trending. Huko YouTube au boomplay sijui. Hivi msanii akitoa Ngoma halafu raia wakaenda kuangalia au kuisikia let's say watu 2m just kuangalia video au kuisikiliza kwa kuwa wamesikia msanii x ametoa ngoma.

Je hiyo 2m views ndo kupendwa hadi watu wanasema ngoma inatrend sana au naomba kueleweshwa.

Maana hata mm huwa mara chache naweza kuta wimbo au video mtandaoni nikaamua kuangalia Tu hii haimaanishi nmeipenda.
 
Kosa lililotokea kaliona, maringo mengi, kuanza kuimba kawaambia wale wakenya waanze kupanda, alafu wakenya kumaliza watu wanamgoja kachelewa kupanda Kama nusu saa ndo anaingia, ye mwenyeji baada ndo aanze kupanda, nyota ndogo alivyokujaga yule alikuwa bado yupo bush akuona mipango ilivyokuwa sijui.
 
Sijawahi kuwa fan wake Ila sidhani kama kaflop kama mnavyosema maana kuna nyimbo kama wote na single again ni mega hit kwa level za Tanzania.

Sema jamaa apunguze mbwembwe za kutaka kuongelewa kila siku pasipo sababu za msingi lakini pia ku-fake hiyo bad boy personality kwa cheap American accent
 
Wote ni bonge la ngoma kaka. Ni wazo la kikubwa, tofauti na ngoma nyingi za mapenzi za hawa watoto wa Bongo Flava. Kingine ile ngoma ni amerudi kwenye Bongo Flava.

Ova
 
Kitu nnachokiona ni hicho mtu ambae hafi kimziki ni Alikiba pekee

True Kiba hakurupuki na nyimbo nyingi zisizoeleweka anaweza akatoa nyimbo 1 ikahit mwaka mf UTU nyimbo ilijua ku trend tena bila kiki za kipumbavu,yy sasa mara aanze kumuongelea ex mara pic ya hamisa,nae hamisa anamchekea chekea jamaa atamuharibia hata kwa huyo mpenzi wake
 
Nyimbo anazotoa hazina mvuto tena na hazishiki number one kwenye platform yoyote mpaka boomplay ambayo inaonewa mpaka na maunderground kwa kushika number one trending.

Watu wanamkimbia kwenye show. Kondegang ndo hivyo imekufa plus kiki zake ndo hivyo hazihit. Hali ikiendelea hivi basi hatutomsikia tena Harmonize.
Harmonize simkubali kbx. But ukweli hapo boomplay ana album mbili kwenye top ten
 
Wote ni bonge la ngoma kaka. Ni wazo la kikubwa, tofauti na ngoma nyingi za mapenzi za hawa watoto wa Bongo Flava. Kingine ile ngoma ni amerudi kwenye Bongo Flava.

Ova
Ile ni pure bongo flava na Ule wimbo hata kama ni hater wa harmonize toka moyoni lazma uukubali.
Lyrics, melody, sauti hadi video. Kila kitu kilikuwa on point mkuu
 
Harmonize ana kipaji kikubwa sana. Mimi ni mmojawapo namkubali sana pia. Tatizo hana management nzuri. Anataka kila kitu afanye yeye.

Watu wengi hamuelewi Daimond kwa nini ana mameneja wengi na anawalipa pesa kibao. Japo hao mameneja yeye anawaongoza cha kufanya,lakini nao wanamuongoza nini afanye kipi aachane nacho. Wale mameneja wa Dai kila mmoja ana kazi yake.

Tatizo lingine kubwa la Harmonize ni kuendelea kufuata upepo wa Dai. Kupambana na Dai ni kujipoteza. Yeye alivyoamua kujichomoa Wasafi. Ilitakiwa awe amejipanga kufanya kazi kwa juhudi bila kugeuka upande wa pili. Ilitakiwa afanye kazi zake kulingana na alivyojipanga tu si vinginevyo.

Mwisho ushauri wangu kwake ni ule ule wa siku zote. Japo utakuwa umechelewa,lakini hakuna namna. Ache kumshambulia Daimond kabisa. Ilipaswa kila anapomuongelea Diamond amuongelee vizuri sana Daimond. Kumuongelea vizuri Dai sio kujishusha ,bali angejiongezea nguvu sana. Angejiongezea pia mashabiki wengine wa upande wa pili wangeendelea kumsapot. Pia ni ishara ya kurudisha fadhira.

Pia ingempunguzia sana maadui wa kupambana nao,badala yake ange-focus kwenye kazi tu. Bila Dai yule dogo nina uhakika asingejulikana kokote. Bila Dai asingekuwa na maisha aliyonayo sasa.

Japo hayo ilitakiwa ayafanye kitambo.
 
Nje ya topic kidogo. Huwa sielewi mtu akisema on trending. Huko YouTube au boomplay sijui. Hivi msanii akitoa Ngoma halafu raia wakaenda kuangalia au kuisikia let's say watu 2m just kuangalia video au kuisikiliza kwa kuwa wamesikia msanii x ametoa ngoma.

Je hiyo 2m views ndo kupendwa hadi watu wanasema ngoma inatrend sana au naomba kueleweshwa.

Maana hata mm huwa mara chache naweza kuta wimbo au video mtandaoni nikaamua kuangalia Tu hii haimaanishi nmeipenda.
Sa unazani kupendwa kwa msanii wanatumia statical way ipi..?
 
Back
Top Bottom