Harmonize ana kipaji kikubwa sana. Mimi ni mmojawapo namkubali sana pia. Tatizo hana management nzuri. Anataka kila kitu afanye yeye.
Watu wengi hamuelewi Daimond kwa nini ana mameneja wengi na anawalipa pesa kibao. Japo hao mameneja yeye anawaongoza cha kufanya,lakini nao wanamuongoza nini afanye kipi aachane nacho. Wale mameneja wa Dai kila mmoja ana kazi yake.
Tatizo lingine kubwa la Harmonize ni kuendelea kufuata upepo wa Dai. Kupambana na Dai ni kujipoteza. Yeye alivyoamua kujichomoa Wasafi. Ilitakiwa awe amejipanga kufanya kazi kwa juhudi bila kugeuka upande wa pili. Ilitakiwa afanye kazi zake kulingana na alivyojipanga tu si vinginevyo.
Mwisho ushauri wangu kwake ni ule ule wa siku zote. Japo utakuwa umechelewa,lakini hakuna namna. Ache kumshambulia Daimond kabisa. Ilipaswa kila anapomuongelea Diamond amuongelee vizuri sana Daimond. Kumuongelea vizuri Dai sio kujishusha ,bali angejiongezea nguvu sana. Angejiongezea pia mashabiki wengine wa upande wa pili wangeendelea kumsapot. Pia ni ishara ya kurudisha fadhira.
Pia ingempunguzia sana maadui wa kupambana nao,badala yake ange-focus kwenye kazi tu. Bila Dai yule dogo nina uhakika asingejulikana kokote. Bila Dai asingekuwa na maisha aliyonayo sasa.
Japo hayo ilitakiwa ayafanye kitambo.