Kumekuwepo graphic ambayo inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii (hasa Facebook) yakidai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche, amethibitisha kuvunjika kwa ndoa ya Tundu Lissu kutokana na mizozo ya mali. Taarifa hiyo imetumia nembo ya chombo cha habari cha Chanzo TV.
- Tunachokijua
- Kumekuwepo graphiki inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii (hasa Facebook) ikidai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche, amethibitisha kuvunjika kwa ndoa ya Tundu Lissu kutokana na mizozo ya mali. Taarifa hiyo imetumia nembo ya chombo cha habari cha Chanzo TV.
Je, uhalisia upoje?
Ufuatiliaji wa kina umethibitisha kuwa Taarifa hiyo ni potofu ikiwa na mlengo wa kutoa taarifa potofu kwa umma.
Baada ya kufanya ufuatiliaji katika kurasa rasmi za Chanzo TV (Twitter/X, Instagram, na Facebook), imebainika kuwa hakuna Taarifa kama hiyo iliyowahi kuchapishwa. Picha inayosambaa imetengenezwa kidijitali (manipulated) kwa kughushi muonekano wa machapisho ya chombo hicho.
Sambamba na hilo makamu mwenyekiti John Heche hajatoa tamko lolote kuhusiana na maisha binafsi ya Tundu Lissu. Kumbukumbu za mahojiano yake ya hivi karibuni ambayo amefanya akiwa na chombo cha habari cha mwananchi na mara baada ya kusikiliza kesi mahakamani yamelenga masuala ya kisiasa na mwenendo wa kesi inayomkabili Tundu lissu
Taarifa hii inatengenezwa ikiwa Tundu Lissu anakabiliwa na changamoto za kisheria (ikiwemo tuhuma za uhaini), na hakuna taarifa rasmi kutoka kwa familia yake au mwanasheria wake inayothibitisha kuwepo kwa mgogoro wa kifamilia.