Si Membe aliyesababisha biashara ya Korosho kudorora, maamuzi ya kukurupuka ndiyo yametufikisha hapa!

Si Membe aliyesababisha biashara ya Korosho kudorora, maamuzi ya kukurupuka ndiyo yametufikisha hapa!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Ni hivi:

Siyo Membe aliyesababisha biashara ya Korosho kudorora huko kusini. Ni maamuzi ya kukurupuka ndiyo yametufikisha hapa.

Ni sawasawa na walivyozuia wanunuaji wa Kahawa kutoka kwa madalali na matokeo yake kujikuta hawawezi kumtosheleza mkulima kwa soko bora na bei nzuri.

Jamani Mkapa alisema siyo kila lililofanywa na serikali za zamani ni la kipuuzi, mengine inafaa kuyachukua kuyaboresha na kusonga mbele, siyo kuweka question mark katika mambo ya maana!.

Asije akatokea mtu katika nchi hii akaingia madarakani akadhani kwamba amegundua matatizo ya watanzania ambayo watangulizi wake hawakuyajua!. Kwa mfano kama hoja ni vyeti feki BWM alikuwa anajua, JK alikuwa anajua. Ila may be hawakuamua kudeal navyo in the first place, au walikosa means za kudeal navyo ktk wakati huo. Huo ni mfano mmoja

Kama hoja ni mikataba mibovu ya serikali za nyuma kila atakayekalia hicho kiti atajua tu kwa sababu naye atakuwa na vyombo vilevile na instruments zilezile ambazo mwingine anazo!

Kwa hiyo cha msingi siyo kujua matatizo yapo au hayapo, HOJA YA MSINGI ni mbili

1. Kutokufanya makosa ambayo yalipelekea matatizo kuwepo in the first place

2. Kuja na mbinu BORA zaidi ya kuyaondoa hayo matatizo!

Wakati mwingine ni bora kusikiliza kauli, hoja na mitizamo mingine ili kuweza kufanya maamuzi yanayotokana na utafiti wa kina.

Ishu ya Korosho wabunge walipiga kelele sana, hawa ni wawakilishi wa wananchi, wanakuwa kule site, wanajua kero za wananchi, ukiwadismiss hawa as if ni wasaliti unadhani wananchi watafurahi?.

Kwa hiyo wananchi wanaona maslahi yao hayasimamiwi ipasavyo na wanaopaswa kuyasimamia. Kumtumbua huyu na yule hakuwezi kusolve ishu au kero ya mkulima.

Mkulima anataka soko la korosho, Pembejeo, Usafiri, Packaging nzuri etc etc. Hivi havipatikani kwa kumtumbua mtu!

Kulaumu watu, na kutafuta bangusilo wa kumtupia lawama haisaidii!

Membe siyo hata mtendaji wa kata, kudhani kwamba eti anakwamisha kwenye ishu ya korosho ni sawa na kupiga penati huku umefumba macho!
 
"Tunaunga mkono juhudi" [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Naomba niwaulize Gekule na Chacha jee mnaunga mkono juhudi za kuua korosho kule kusini?
Hakika nawaambia katiba yetu kama ingekuwa inaruhusu wabunge kuhama vyama vyao na ubunge wao basi wale 17 wa kusini ambao mashangazi zao wangenyukwa kwa wao kutetea korosho wangehama.
Hii ingeambatana na wengi waliochoshwa na Jiwe na kubaki hawa wa Polepole wanaounga mkono juhudi kwa ahadi za kuukata
 
mkuu, very stupid habit tumejengewa... mwenye mamlaka anamtupia lawama asiye na mamlaka. Wana maaskari. watunga sera, wataalamu wa masoko, wataalamu wa kilimo, wadukuzi wa maswala ya biashara lakini bado wanahisi wanahujumiwa na mtu ambae hajawahi hata kufanya press conference tangu waingie madarakani.
 
Kwani Mkulu amesema Membe ndiye kasabbaisha hayo? amesema Bodi ya Korosho ijitathimini na Wizara ya Kilimo ijitathimini kwisha PM kaagizwa mnada hautafanyika mpaka pale watakapo tangaza tena.
 
Kawaida ya watu wasiojua nini wafanye kutatua tatizo,huwa wanatafuta wa kumbebesha lawama
 
Ni sawasawa na walivyozuia wanunuaji wa Kahawa kutoka kwa madalali na matokeo yake kujikuta hawawezi kumtosheleza mkulima kwa soko bora na bei nzuri.
Katika Kahawa upo sawa ila korosho haupo sawa, sisi wamaraba tunasema una Manga Manga au kutindinganya Mambo
 
Hii ishu ya korosho isipokuwa handled vizuri inaweza kupelekea kuporomoka kwa uzalishaji wa zao la korosho kwa kiwango ambacho hatujawahi kushuhudia
 
hivi na sisi tunaopata tabu kwa kutolipwa mafao yetu ya kustaafu tumlaumu nani?au inatakiwa kuunga mkono kutolipwa mafao yetu?
 
Back
Top Bottom