Si Membe aliyesababisha biashara ya Korosho kudorora, maamuzi ya kukurupuka ndiyo yametufikisha hapa!

Si Membe aliyesababisha biashara ya Korosho kudorora, maamuzi ya kukurupuka ndiyo yametufikisha hapa!

Siku ambayo Lubuva alibuni matokeo na kumteua huyu jamaa wa chattle ndio ulikuwa mwanzo wa kuirudisha Tanzania miaka 100 nyuma kabla ya uhuru.
 
hivi na sisi tunaopata tabu kwa kutolipwa mafao yetu ya kustaafu tumlaumu nani?au inatakiwa kuunga mkono kutolipwa mafao yetu?
Yaani mambo katika awamu hii yanakwenda ovyo kila upande........

Fao la kujitoa wameamua "kuwapora" wafanyakazi na kulipeleka Hazina......

Export levy ya korosho wameanua "kuwapora" wakulima wa korosho na kuzipeleka Hazina......

Yaani nchi hii tulikosea sana kumpa kiongozi kichaa kutuongoza.....

Yaani yajayo yanasikitisha sana!
 
Kuanzia mkuu wa kaya, VP, Dokta mpaka Majaliwa woote hawa wamekuwa wakipokea mshahara tangia mwanzo wa ujana wao mpaka kaburini, sasa unategemea sekta ya biashara itanawirishwa chini ya mikono ya mtu/watu waliolemazwa na mishahara?!!

Ulichoongea kinafikirisha sana!
 
Ni hivi:

Siyo Membe aliyesababisha biashara ya Korosho kudorora huko kusini. Ni maamuzi ya kukurupuka ndiyo yametufikisha hapa.

Ni sawasawa na walivyozuia wanunuaji wa Kahawa kutoka kwa madalali na matokeo yake kujikuta hawawezi kumtosheleza mkulima kwa soko bora na bei nzuri.

Jamani Mkapa alisema siyo kila lililofanywa na serikali za zamani ni la kipuuzi, mengine inafaa kuyachukua kuyaboresha na kusonga mbele, siyo kuweka question mark katika mambo ya maana!.

Asije akatokea mtu katika nchi hii akaingia madarakani akadhani kwamba amegundua matatizo ya watanzania ambayo watangulizi wake hawakuyajua!. Kwa mfano kama hoja ni vyeti feki BWM alikuwa anajua, JK alikuwa anajua. Ila may be hawakuamua kudeal navyo in the first place, au walikosa means za kudeal navyo ktk wakati huo. Huo ni mfano mmoja

Kama hoja ni mikataba mibovu ya serikali za nyuma kila atakayekalia hicho kiti atajua tu kwa sababu naye atakuwa na vyombo vilevile na instruments zilezile ambazo mwingine anazo!

Kwa hiyo cha msingi siyo kujua matatizo yapo au hayapo, HOJA YA MSINGI ni mbili

1. Kutokufanya makosa ambayo yalipelekea matatizo kuwepo in the first place

2. Kuja na mbinu BORA zaidi ya kuyaondoa hayo matatizo!

Wakati mwingine ni bora kusikiliza kauli, hoja na mitizamo mingine ili kuweza kufanya maamuzi yanayotokana na utafiti wa kina.

Ishu ya Korosho wabunge walipiga kelele sana, hawa ni wawakilishi wa wananchi, wanakuwa kule site, wanajua kero za wananchi, ukiwadismiss hawa as if ni wasaliti unadhani wananchi watafurahi?.

Kwa hiyo wananchi wanaona maslahi yao hayasimamiwi ipasavyo na wanaopaswa kuyasimamia. Kumtumbua huyu na yule hakuwezi kusolve ishu au kero ya mkulima.

Mkulima anataka soko la korosho, Pembejeo, Usafiri, Packaging nzuri etc etc. Hivi havipatikani kwa kumtumbua mtu!

Kulaumu watu, na kutafuta bangusilo wa kumtupia lawama haisaidii!

Membe siyo hata mtendaji wa kata, kudhani kwamba eti anakwamisha kwenye ishu ya korosho ni sawa na kupiga penati huku umefumba macho!
Membe wa G Sam anafikaje hapa?
 
bei ya korosho haiwezi kuwa nzuri mpaka tuwe na viwanda vya maana vya kubangua korosho, wengi walionunua viwanda wamevigeuza maghala kwa mtindo huu wa kuuza korosho ghafi lazima bei haitakuwa imara
 
Safi sana kudadeki ! Mtashikana uchawi mpaka siku Yesu anarudi .
 
Hii ishu ya korosho isipokuwa handled vizuri inaweza kupelekea kuporomoka kwa uzalishaji wa zao la korosho kwa kiwango ambacho hatujawahi kushuhudia
Korosho sio mara ya kwanza kuporomoka au kupanda.Mikoa isiopungua 16 imeanza kulima zao hilo,ni wazi sababu ya wingi wa washiriki tutapata wingi wa zao hilo,tutegemee siku za usoni tukapata ufumbuzi wa kudumu kwa kubangua korosho zetu hapa nchini ili kuongeza bei ya zao hilo.
 
hapa tukubaliane jambo moja, mtazamo wetu Kwenye kilImo unabidi tuutazame upya;
1) tunalima nini ? koroshi
2) soko la ndani ni kubwa kiasi gani ukilinganisha Na la nje la aina Na Quality tulizo nazo?
3) washindani wetu wakuu watatu sokoni wanapeleka quantity, Quality Na Price gani gani ?,critical Price(BEP) yao ningapi kabla wakulima wao hawajapata hasara ?
4)Tuna competitive advantage gani juu ya hoa washindani wetu huko sokoni?Kama hatuna tunaitengeneza.
mfano uliofanyika ila zao tofauti : mawese
mzalishaji mkubwa sana duniani alitumia njia Hii akagundua ana advantage ya land peke na wakulima tu.
akatengeneza mbegu zake( hybrid ) uzao wa mbegu alitoa Wapi ?kigoma - Tanzania.
matokeo ;
dunia nzima inanunua mbegu kutoka kwake hata sisi tutafanya hivyo maana zake ni Bora kuliko zetu kwa sasa!

5) udhibiti wa bei, tuwatazame wachina
wachina hawauzi BEP quantity Kama export, wanauza extra capacity Kama export. kwa nini ?
ukiuza BEP Na profit qty Kama export mvurugano Was oko la dunia una muathiri mkulima wako maana anategemea hilo soko kuishi,wakati ukiusza excess Kama hilipi anaacha,kwa wachina kazi ya serekali ni kutengeneza masoko yote ya ndani Na nje, iliwakulima wakimbize uzalishaji. wakibashiri mara wameuza mahindi vibaya sereekali inaingIasokoni Kama mteja wa kawaida inanunia kwa Bei ya soko kulinda wakulima wa kibaigwa wasipate hasara, serekali inapeleka mahindi yake mara,shotage ikitokea inayaingiza sokoni mara hakuna njaa hapo. wakulima wengine hawaoni hilo tatizo la mara ila wahusika wa uzalishaji mkoa hio wanatakuwa wazidishe uzalishaji Na elimu kwa wakulima kuhusu hifadhi ya chakula.Hii ni mazao ya biashara Na ya chakula.

6) jambolingine ni gereric foods Na natural foods :
generic foods kilamtu anazo Wewe unaweza maintain original breed yako Na kutengeneza soko lako ( niche market ).

tukitazama Mbele tunaweza fanya vizuri sana hata Kwenye Korosho bila kuingiza siasa za vyama,siasa ibaki kuwa njia ya kupata viongozi utaalamu ubaki utaalamu!
 
bei ya korosho haiwezi kuwa nzuri mpaka tuwe na viwanda vya maana vya kubangua korosho, wengi walionunua viwanda wamevigeuza maghala kwa mtindo huu wa kuuza korosho ghafi lazima bei haitakuwa imara
huu ni utaalamu wa kutawala soko( market management ) ,mteneneza kiwanda akiwa mnunuaji wako mkubwa anakuchezea usitoke, anakuuzia kiwanda kikifika kwako anabadili mahitaji. kiwanda kina kuwa ghala lakuhijfadhi mazao,yeye anataka ghafi Na Bei yake hutaki acha mkulima wako hawezi acha uza hawezi kuzila zote!, unachofanya unajenga kwanza soko la ndani liwe imara sana!
 
"CHADEMA NDIO WAMESABABISHA BEI YA KOROSHO KUDORORA ILI KUMCHONGANISHA MTUKUFU SANA JIWE/KICHAA NA WATANZANIA WANYONGE"
NIMEWAZA KWA AKILI YA BWANA MUSIBA
 
Na watu wenye akili finyu huwa wababe sana na hutaka sana kusifiwa.
1540628405587.jpeg
 
Kwani kipindi Membe yuko kwenye System bei ya korosho ilikuwa Tsh ngapi mpaka ionekane yeye ndite chanzo cha bei kushuka?
 
Back
Top Bottom