hhahahaha yani unacheka, kumbe hukukutana na walimu makauzu
Ivi Rutta wakati huo ulikua una miaka mingapi??
Maana kama ndio miaka 17 ivi yani sipati picha ukiwa na manywele yako kifuani...
mwenzangu huyo wako kazidi.... Kauzu kama dagaaa lol!!!!!!!!
hahaaaa umenichekeshaje.....
Ruttashobolwa wale walimu wetu walikuwa wanakuadhibu,
ila adhabu yako imenichekesha,nimejikuta nacheka tu
Kizazi cha digitali kikifanyiwa na mwalimu hivyo kimeshapiga simu Takukuru,Polisi na waandishi wa habari wanataarifa kikidai kimenyanyaswa na mwalimu .......
daaa huyu Mwl wangu alikuwa kauzu sana na alikuwa akipewa zawadi ya kufahurisha, kwakweli ukipitia kwenye mikono yake lazima unyooke, na wala sikusema nyumbani maana walikuwa wanamfahamu na kumsifia kwa kujua kucontrol wanafunzi,
umenikumbusha mwalimu wangu wa French wakati niko secondary....... Naye alikuwa kauzu ka nini, hadi nilitamani kutoingia kwenye pindi lake.....! Ila sasa najuta kwanini nilikuwa nampuuzia!!!!!!!!
Mkuu.
Umenikumbusha mwalimu wangu wa Hisabati darasa la Tatu. Alitoa swali akasema "anayejua apite afanye ubaoni". Mtu mzima nikajipitisha, dah! nikashindwa kulifanya. Nilistukia bonge la kofi, akasema "nimesoma wanaojua, kama haujui kakae"
Niliumia sana rohoni. Alinifanya kuwa muoga wa kujaribu mambo.
Kuna wakati hata kuwatongoza wasichana nilikuwa naogopa. Aliniathiri kiakili.
Ruttashobolwahahahaha pole sana Mzee wakati mwingine si kila wanayo tufanyia walimu yanatusaidia, mengine yanatuathiri.
I hope your ok now
Umezidi kuvunja mbavu zangu . Yaani nimecheka sana nikamkumbuka mwl wa somo la sayansi lol. Jamani zamani walimu walikua na moyo sanaHahahahahahaaa.......... Yaani nimecheka mpaka nimelia... Na shati lingejaa ungeandika mapajani then usahishiwe......!