Si sahihi kufikiri eti komandoo akiwa mtaani ni kama raia wa kawaida

Fikiri ivo ila siku akikufumania ndo utajua hujui
 
hapa tz kuamini kuwa hakuna aliye juu ya sheria ni sawa na kujilisha upepo.
Tumeona Ole Sabaya (DC), Freeman Mbowe (VIP) na makomandoo kadhaa sheria inavyowashughulikia. Au unataka uwaone na akina nani ndiyo uamini kuwa hakuna aliye juu ya sheria nchini kwetu?
 
Sio makomandoo tu, hata walimu, madaktari, madereva na wabeba mizigo wote wanastahili heshima wawapo uraiani. Na wakikokesea, sheria inafuata mkondo.
 
Ugaidi mbona unausema ww, Kingai na Mahita umewasikia wakiutaja,[emoji1745]
Ugaidi ndiyo kesi kuu iliyoko mahakamani. Sasa hivi kinachoendelea mahakamani ni kesi ndogo inayohusu ukamataji wa makamandoo kama ulifuata taratibu za kisheria. Yaani taratibu za polisi kumkamata komandoo ni sawa na taratibu za kumkamata mwizi wa kuku? Hiki ndicho kimekuwa kikibishaniwa mahakamani kwa wiki 2 hadi sasa. Jaji atatoa hukumu ya ubishi huu tarehe 15 October. Kesi kuu wala haijaanza. Mawakili wa Mbowe wanavuta tu muda ili kesi ichukua muda mrefu zaidi na gharama kuwa kubwa zaidi kwa chadema kuwalipa hao mawakili 16 kwa kipindi chote hicho!
 
Hivi mnafikiri ugaidi ni suala la polisi pekee kwa sababu ndo mnawaona huko mahakamani?majeshi yote yana wajibu huo
 
kwani wewe pgo unaijua??

ni sahihi kusema hujui wala huwezi kufanya mambo mengine kwa usahihi!!!!!
Sasa boss kwani mie Polisi mpaka niijue PGO? Huo ndio msaafu wao, ndio kitu cha kwanza kukijua kabla hata hujajua kucheza paredi
 
Tumeona Ole Sabaya (DC), Freeman Mbowe (VIP) na makomandoo kadhaa sheria inavyowashughulikia. Au unataka uwaone na akina nani ndiyo uamini kuwa hakuna aliye juu ya sheria nchini kwetu?
Umeona hao tuu ili kuhalalisha mfano wako butu?
 
Mabavicha ya mnatafuta huruma kwa jwtz
 
Ndio Maana hakuna mwanajeshi yeyote Nchii hii anamsema Vizuri Polisi kama ulipata nafasi ya kufika Jkt hata kwenye mafunzo utalitambua hilo au hata kama umepata mda wakupiga nao stori wanajeshi na makomandoo utajua jinsi gani hawa watu wanawaona Polisi Vibwengo..

Kuna mda wanawaita Mashangazi😂😂😂😂
 
Nina wasiwasi Jeshi JWTZ linafuatilia kwa karibu mienendo ya Jeshi la polisi,kwani ndani ya JWTZ wapo wenye uelewa na wanaofuatilia siasa za nchi yetu,itakuwa wanahesabu zao na mipaka yao,labda polisi hawajaivuka.
 
Miye nawaA tu makomando watatu hata kama aaskari walikuwa na silaha za moto walishindwaje wamudu huo ukomando wao vipi nawaza naona huo ukomando wa kudesa siyo wavitendo
Acha kutumia akili za kitoto,lazima ufikilie mbele .Baada ya makomando kuwapiga polisi huoni kesi ya mbowe ingekuwa imeisha angehukumiwa?. Vilevile askari wazalendo na wanyenyekevu ktk nchi hii wanajeshi namba Moja.Mafunzo yao ni kulinda nchi na mipaka na si kupigana na kina kingai .You must think carefully before you put your actions ahead as a gentleman
 
Mbona wewe umeiongelea hiyo kesi wakati unafahamu iko mahakamani?
 
Sasa wavaa vitenge wana kipi hasa kuwazidi hao polisi? Wanajeshi nimewadharau kuanzia leo tena hao makomando ndio taka taka kabisa,mavi ya popo.Maigizo yao ya kuvunja tofali pale taifa nilidhani ni 'untouchable' kumbe ni wala chipsi.Gaidi Kingai na Mahita wamewadaka kama kuku wa mdondo pamoja na hayo polisi wamewafanya watakavyo.TZ hatuna wanajeshi wala makomando bali tuna uharo.[emoji1]
 
Sasa boss kwani mie Polisi mpaka niijue PGO? Huo ndio msaafu wao, ndio kitu cha kwanza kukijua kabla hata hujajua kucheza paredi

mkuu askofu au sheikh kutenda dhambi haimaanishi hajasoma kitabu anachokifundisha.

upo wakati kiburi cha binaadamu au mazingira humlazimisha kufanya dhambi aliyofanya.

hucho kitabu unachosema hawakijui bahati mbaya nawewe hujui hata kinazungumzia nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…