Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Wakili Maarufu nchini,Alex Mgongolwa amekosoa kitendo cha Serikali kutimiza siku ya saba bila ya kuwapo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akisema si sahihi. Amesema licha ya kwamba yupo Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,bado kuna umuhimu wa kuwapo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwasababu kuna mambo ambayo ndiye anayepaswa kuyaamua au kuyasimamia na si Naibu wake.
Mgongolwa alisema " Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni nafasi nyeti na kulingana na utendaji wake wa kazi kikatiba si jambo zuri nchi kukaa takribani wiki mbili bila kuwa naye" Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye mshauri wa Serikali juu ya mambo ya sheria na pia anatekeleza shughuli nyingine zinazohusiana na sheria zinazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza. Pia ni Mbunge na ana haki ya kuhudhuria na kusikilizwa na Mamlaka zote katika Jamhuri ya Muungano.
Chanzo: Mwanachi,uk.3