Pre GE2025 Si sahihi Mwanaccm Kuomba Rais Samia aongezewe muda hadi 2030, Kwa Mujibu wa Utamaduni wa CCM Rais Samia anaendelea hadi 2030 kihalali bila kuombewa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nilitaka niliweke hilo sawa kwamba kwa mujibu wa utamaduni wa CCM Rais anahudumu term 2 kama Katiba ya JMT inavyotaka

Sasa akiibuka mwanaccm sasa na Kuomba Rais Samia aongezewe muda hadi 2030 tunamshangaa kwa sababu huo ndio utamaduni sasa wewe unaomba ukimaanisha nini

Ni hilo tu

Ahsanteni πŸ˜€
 
Magu: Marais waliopita wote waliongoza Awamu mbili kwanini Mimi mnipe Awamu Moja pekee?

Hii kauli nilijiuliza sana, alikuwa anaongea na nani ilhali Yeye ndiye Rais na mgombea Urais pekee.

Sasa ikiwa Magu aliongoza Awamu Moja, kwanini ushangae sa100 pia kuongoza Moja Kisha Akaenda kulea wajukuu?
 
Case ya rais Samia ni special. Aligombea na mwenzake 2015 na 2020. Baada ya mwenzake kufariki yeye akakabidhiwa amalizie ungwe yao mpaka 2025.

Japo katiba ya nchi inamruhusu kugombea muhula mmoja zaidi, hiyo haiondoi ukweli kwamba chama hakijawahi kumpima na kumridhia kwa nafasi hii ya sasa anayomalizia. Hivyo 2025 anaweza kuwekwa kwenye mzani na akaonekana hatoshi.
 
Sisi ndani ya CCM tulishamaliza mchakato bwashee Uchaguzi wa Rais ni 2030

Sasa tunashughulika tupate Wabunge tu na Madiwani wa kutosha
 
Kwa mawazo tofauti lakini. Katiba ya JMT inasemaje. Kipindi cha mpito na baada ya hapo inakuwaje.Katiba ya CCM inasemaje ? Je hatuna utashi wa kuondoa mikanganyiko hiii?
 
Atakuwa alimaanisha aongezewe hadi 2035.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…